Vijana hawana shukrani-Lukamba akashifiwa na blogu kwa kumdharau Diamond

Lukamba alikuwa mpiga picha wake rasmi lakini kwa sasa aliondoka na kuanzisha kampuni yake.

Muhtasari
  • Diamond anamiliki rekodi kubwa zaidi nchini Tanzania . Lebo ya Wasafi imekuza miongoni mwa wasanii wakubwa wa Tanzania
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Diamond Platinumz ni msanii maarufu wa Tanzania na miongoni mwa wasanii wa kimataifa wanaojulikana kwa kuimba kwa lugha ya mama.

Ni baba wa watoto wanne.

Diamond anamiliki rekodi kubwa zaidi nchini Tanzania . Lebo ya Wasafi imekuza miongoni mwa wasanii wakubwa wa Tanzania.

Hawa ni pamoja na Harmonize, Lukamba, Rayvanny, Richard Mavoko, mboso na Zuchu miongoni mwa wengine.

Hata hivyo licha ya yeye kuwasaidia kupitia msanii huyo wameiacha label hiyo wengine wakiwa katika hali nzuri wengine wakiwa katika hali mbaya .

Lukamba ni miongoni mwa wasanii ambao wameachana na Wasafi kwenye mahusiano mabaya na bosi wake .

Leo msanii huyo amekashifiwa na moja ya kurasa maarufu za blogu nchini Tanzania.

Hii ni kwa tabia yake ya kutokuwa na shukrani aliyoionyesha kwa bosi wake hata baada ya kupokea gari kutoka kwake.

Lukamba alikuwa mpiga picha wake rasmi lakini kwa sasa aliondoka na kuanzisha kampuni yake.

"Lukamba aliliaa sanaa alivyopewa gari na simba ila leo anamdharau hawa vijana hawa hawana shukrani kabisa 😅😅😅😅."