Natalia Florence, wengi wanamjua kama Notiflow, ni msanii ambaye alikuwa na kipaji cha kutema mistari ya rao sana ila baada ya kuingia katika dunia ya mapenzi, imechukua muda mrefu sana kwa mashabiki zake kusikia ngoma mpya kutoka kwake.
Msanii huyo ambaye muda fulani nyuma aliweka wazi kwamba yeye ni shoga na hata kuanika hadharani mapenzi yao na mrembo King Alami, alikuja akasema kwamba wameachana, miezi michache tu baada ya kununuliana gari kama zawadi na mrembo huyo mpenzi wake.
Alikawia kwa muda kabla ya wiki chache zilizopita kumtambulisha tena mrembo mpenzi wake kupitia mtandao wa Instagram.
Ila tena kwa bahati mbaya siku kadhaa baada ya utambulisho huo, Notiflow alitangaza kuvunjika kwa huba lake na mrembo huyo na kuweka wazi kwamba yupo singo. Alidokeza kupitia instastories zake kwa ujumbe wa kuonesha mambo hayakuenda sawa jinsi alivyofikiria na ndio maana akaamua kuachia.
Wikendi iliyopita tena amedokeza kwamba huenda amepata mrembo mpya, wiki moja tu baada ya kutengana na mrembo mwingine ambaye hakusema jina lake awali.
Kupitia instastories zake, Notiflow wikendi iliyopota alidokeza kwamba yeye ni mrembo sana kukawia sokoni kwani anaingia tu hivi na kupata mnunuzi haraka kutokana na kubarikiwa kwa urembo.
Katika stori hiyo, Notiflow alipakia picha ya mikono, mmoja wake na mwingine wa huyo mpenzi mpya wakikwa wameshikana akisema kwamba yeye ni kuingia soko na kutoka wala hakawii.
“Mimi ni mrembo sana kukaa singo, ni kuingia soko na kutoka,” Notiflow aliandika kwenye video ya TikTok.