MSANII ARROWBOY AWAHIMIZA VIJANA KUTUMIA KINGA

Arrow Boy amewashauri wanaume ambao hawako tayari na ulezi kutumiia kinga

Muhtasari

•Arrow boy amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki Nadia Mukami kwa muda sasa.

•Aliweka wazi kwamba mchumba wake Arrow Boy amekuwa akisaidia sana katika kushughulikia mtoto wao .

Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAMI

Staa wa kimaarufu wa mziki Ali Yusu alimaarufu, Arrow Boy amewashauri wanaume ambao hawako tayari na ulezi kutumiia kinga katika pilkapilka zao za matendo ya mapenzi.

Amewapa wanaume tahadhari za mbwe mbwe za safari ya mwanamke kuubeba uja uzito kwa miezi tisa na kuwa sio rahisi.

Hata hivyo msanii huyo aliwahimiza wanaume kuwa wakijipata kwenye hali hiyo wakubali kushirikiana na wapenzi wao kulea mtoto wao.

Arrow boy amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki Nadia Mukami kwa muda sasa.

Arrow Bwoy na Nadia walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Machi 24 mwaka huu.

Miezi miwili iliyopita mama huyo wa mtoto mmoja alifichua kuwa miezi minne baada ya kujifungua mwanawe haijakuwa rahisi kwake.

 

"Kipindi cha baada ya kujifungua sio mzaha! Sikuwahi kuelewa kabisa kuhusu kipindi cha baada ya kujifungua hadi nilipopata mtoto," Alisema kupitia Instastori zake.

 

Mpenzi wake Arrow boy pia alibainisha kuwa kipindi cha baada ya kujifungua kwa kawaida huwachosha wanawake wengi.

Kulingana naye, kipindi cha ujauzito huwa rahisi kwa mwanamke kuliko kipindi cha baada ya kujifungua.

"Ujauzito ni rahisi! (Maoni yangu) nadhani ni rahisi ukilinganisha na kipindi kile baada ya kujifungua! Sheesh! Wanawake wana nguvu! Na sisi wanawake weusi/Waafrika haturuhusiwi kusema kipindi hiki kinachosha utaambiwa , leta mtoto ni/tulee kama amekushinda," Nadia alisema.

Hapo awali wapenzi hao walikuwa wamepoteza ujauzito wa ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza.

Hata hivyo, Nadia alibahatika kupata ujauzito mwingine takriban miezi miwili baada ya kupoteza ule wa kwanza.


Wawili hao wametoa ngoma ili kumpa heshima na sifa njema kifungua mimba wao waliyemwita Kai.

Miezi mitano iliyopita Nadia alifichua kuwa angependa kupata watoto wengine wawili ili kufunga ukurasa wa kuzaa.

Aliweka wazi kwamba mchumba wake Arrow Boy amekuwa akisaidia sana katika kushughulikia mtoto wao .

"Nina furaha na nashukuru kuwa yeye ni baby daddy wangu na mchumba. (Arrow Bwoy) Yeye ni baba mzuri. Ameosha mwanawe mara nyingi kuniliko kufikia sasa walahhi," Alisema Nadia.