Jeneza dogo zaidi ndilo zito zaidi - Kambua aachia ujumbe wenye hisia

Kambua pia aliwahimiza watu kuwajulia hali wanadada walioharibikiwa na uja uzito

Muhtasari

•“Wapigieni, watumieni ujumbe sasa hivi mkiweza,”alisema.

Mwinjilisti Kambua
Mwinjilisti Kambua
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Kambua aliweka mtandaoni kuwa jeneza dogo huwa zito zaidi.

Msanii huyo hata hivyo hakueleza sababu yake ya kuandika hivyo. Alisema hataweza kueleza alichokuwa anamaanisha kwa sasa ila siku za mbeleni ataweza kujieleza.

Kambua pia aliwahimiza watu kuwajulia hali wanadada walioharibikiwa na uja uzito na wale ambao walijifungua watoto waliokata roho.

Mwimbaji huyo aliwaambiwa watu wawaoneshe upendo, bila kusahau kuwaambia wanapendwa na kuwa wana watu wa kuwajali.

“Wapigieni, watumieni ujumbe sasa hivi mkiweza,”alisema.

Kando na hayo alisema pia wakiwajulia hali wanadada hawa ,watu wawakumbushe kuwa watoto wao amabo hawangeweza kuwa pamoja nao walikuwa muhimu.

Kambua ni mama ya watoto wawili, mmoja akiitwa Nate, mwengine aliyekata kamba siku chache baada ya kuzaliwa.

Siku ya akina mama mwaka huu, mwinjilisti huyo alisema kuwa ana hisia mbalimbali zilizokuja na siku hiyo.

Alikuwa na hisia chungutamu za kuwa na mwanawe mikononi na kando yake, na kumbukumbu za mwengine akipumzika mbinguni.

Kambua alifafanua na kusema kuwa alihisi ni kama amekabwa ila bado alijiskia mchangamfu na mwenye uhai .

“Nimelia sana, machozi mengi sana na nashukuru kwa safari hii ya miujiza niliyomo,”alisema.

Pia aliwaandikia wanawake waliojipata kwenye hali ya bahati mbaya ya kuelewa hisia za kupoteza mtoto.

“Kwa wanawake ambao hawajaweza kupata ujauzito wowote ila wamekuwa wakiona siku ya akina mama ikisherehekewa, wale ambao wamekuwa wakitamani zaidi ya mtoto mmoja kwa muda mrefu, wale wanaolea mtoto wa mwengine na kwa njia moja au nyingine mmeweza kuwadunisha kwa sababu ya hisia zinaowavunja, mnapendwa,” Kambua alisema.

Aliwanyooshea mkono wake wa upendo wanawake wanaojikaza kuwa sawa ingawa uzazi umewavunja roho kwa njia zote zile.

“Mnaonekana na mnatosha, kutoka rohoni mwangu mpaka kwa yenu,”alisema.

Siku tatu zilizopita, Kambua aliweka uchapisho uliodhihirisha kumkumbusha kuwa anawezana na jambo lolote.