Nataka kuwa mtu wa kwanza kumwambia kilichomfanyikia baba yake- Matete afichua hofu yake kuu

Ruth alisema kwamba anahisi baadhi ya watu hawampendi,ata baada ya habari za kifo cha mumewe kuwekwa bayana.

Muhtasari
  • Kulingana na Ruth ana hofu jinsi mwanawe ata hisi baada ya madai ya uongo kwamba alimuua mumewe
ruthmatete
ruthmatete

Msanii wa nyimbo za injili Ruth Matete, kupitia kwenye Youtube amefichua hofu yake kuu, baada ya mwanawe kukua.

Kulingana na Ruth ana hofu jinsi mwanawe ata hisi baada ya madai ya uongo kwamba alimuua mumewe.

Mumewe msanii huyo aliaga dunia Aprili 2020, baada ya kuchomeka na gesi akiwa nyumbani.

"Mimi huogopa kuwa siku moja atatoka pale nje ,kisha mtu amwambie kwaba nilimuua baba yake

Kwa hivyo wakatii mwingine hufikiria kuhusu mambo hayo, na nataka kuwa wa kwanza kumwambia kichomtendekea baba yake,natamani baba yak angekuwa hapa ili mtoto ahisi upendo wa mama na baba

Nan mambo haya ya kidigitali napaswa kuanza mapema ili wakati atajua mambo nitamjulisha," Alizungumza Ruth.

Ruth alisema kwamba anahisi baadhi ya watu hawampendi,ata baada ya  habari za kifo cha mumewe kuwekwa bayana.

Msanii huyo alirejelea yale yalitendeka wakati wa tukio hilo la kuhuzunisha.