Fahamu wanaume waliotoka kimapenzi na Wema Sepetu kabla ya Whozu

Wema na Diamond walikuwa kwenye mahusiano yaliyokumbwa na madai kadhaa ya kuchepuka.

Muhtasari

•Wema Sepetu alitangaza mahusiano yake mapya na Whozu mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake

•Wema aliwahi kufichua kuwa marehemu Steven Kanumba ndiye alikuwa mpenzi wake wa kwanza wa kweli.

•Wema alichumbiana kwa muda na muigizaji mwenzake Iddris Sultan kabla ya kutengana kwao mwaka wa 2016.

Wawili hao wamethibitisha mahusiano yao.
Wema Sepetu na mpenzi wake mpya Whozu Wawili hao wamethibitisha mahusiano yao.
Image: INSTAGRAM// WEMA SEPETU

Ni wazi kuwa kwa sasa muigizaji maarufu wa Bongo Wema Sepetu anaogelea kwenye dibwi kubwa la mahaba.

Mlimbwende huyo mwenye umri wa miaka 32 alitangaza mahusiano yake mapya na Whozu mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake. Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa muda ila hawakuwahi kufichua.

"Kwa muda mrefu nimekuwa sina raha. Nimekuwana huzuni, nimekuwa  nikilia lakini tangu nilipokutana na Chibaba wangu (Whozu) nimekuwa na raha na amekuwa akiweka tabasamu kwenye uso wangu," Wema alisema katika video ya moja kwa moja iliyopeperushwa kwenye YouTube usiku wa kuamkia Jumatano.

Wema na Whozu wamekuwa wakijificha chini ya 'urafiki' hadi hatimaye kufikia kufichua mahusiao yao.

Whozu hata hivyo sio mwanaume wa kwanza kuwa katika maisha ya muigizaji huyo. Hapa chini tunaangazia baadhi ya wanaume ambao amewahi kuchumbiana nao katika miaka ya awali.

Image: INSTAGRAM// WEMA SEPETU

1. Steven Kanumba

Miaka kadhaa iliyopita Wema aliwahi kufichua kuwa marehemu Steven Kanumba ndiye alikuwa mpenzi wake wa kwanza wa kweli.

Wema alichumbiana na muigizaji huyo kwa muda kabla ya kukumbana na kifo chake mwongo mmoja uliopita. Wakati huo alikuwa kijana mdogo tu aliyekuwa akijenga taaluma yake ya uigizaji.

2. TID

Miaka kadhaa kabla ya kukutana na Kanumba, Wema alichumbiana kwa muda na mwimbaji wa Bonge mkongwe TID

Wawili hao walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2006 wakati Wema alipokuwa Miss Tanzania.

3. Diamond Platnumz

Wema Sepetu na Diamond Platnumz
Wema Sepetu na Diamond Platnumz
Image: HISANI

Wema Sepetu na staa wa Bongo Diamond Platnumz walichumbiana kwa kipindi kirefu kabla ya mahusiano yao kufika kikomo mwaka wa 2014.

Wasanii hao walikuwa kwenye mahusiano ya msimu yaliyokumbwa na madai kadhaa ya kuchepuka. Hata hivyo waliendelea kuchumbiana hadi Diamond alipokutana na Zari na hatimaye kumtema muigizaji huyo.

4. Ommy Dimpoz

Wema na mwanamuziki Ommy Dimpoz walidaiwa kuwa kwenye mahusiano kipindi kifupi baada ya muigizaji huyo kutengana na Diamond.

Matendo ya wawili hao pamoja na jumbe tamu walizoandikiana zilifanya watu kuamini kuwa wanachumbiana. Baadae hata hivyo Dimpoz alikanusha madai ya mahusiano na kudai walikuwa wakifanya kazi pamoja.

5. Luis Munana

Wema alikutana na mwanamitindo wa Namibia Luis Munana takriban mwaka moja baada ya kutengana na Diamond.

Baada ya kipindi kifupi alitengana naye kwa sababu hakuweza kumudu uhusiano wao wa mbali na baadae akakutana na Iddris Sultan. 

6. Iddris Sultan

wakati wa mahusiano yao.
Iddriss Sultan na Wema Sepetu wakati wa mahusiano yao.
Image: HISANI

Wema alichumbiana kwa muda na muigizaji mwenzake Iddris Sultan kabla ya kutengana kwao mwaka wa 2016.

Licha ya mahusiano yao kugonga mwamba miaka mingi iliyopita wawili hao wamebaki kuwa marafiki wa karibu.

7. Calisah

Wema na mwanamitindo wa Bongo, Calisah walichumbiana kwa muda takriban miaka miaka 6 iliyopita kabla ya mahusiano yao kusambaratika katika njia ya kushangaza sana.

Wawili hao walitengana baada ya Calisah kudaiwa kuvunjisha video yao kwenye mitandao ya kijamii.

8. Chaz Baba

Wema na msanii wa Bongo Charles Gabriel almaarufu 'Chaz Baba' walikuwa kwenye mahusiano ya kipindi kifupi miaka kadhaa iliyotipa. Muigizaji huyo aliwahi kudaiwa kumshambulia mpenzi huyo wake wa zamani kwa kofi.