logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Acha kuniambia eti niliongeza makalio kupitia upasuaji, eti mimi ndio 'next' - Lady Risper

Acha kuniambia kuwa mimi ndio nitafuata, mimi sikufanya upasuaji wa kuongeza makalio - Lady Risper.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 October 2022 - 09:26

Muhtasari


  • • Nilifanyiwa liposuction ili kuondoa mafuta mengi tumboni baada ya kujifungua, sikuwahi kufanyiwa upasuaji kwenye makalio yangu - Lady Risper.
Risper faithc awakomesha wanamwambia kuwa yeye ndiye anafuata Vera sidika kupunguza uzito

Mwanasosholaiti Risper Faith almaarufu Lady Risper ametoka pangoni na kuwarushia dongo mashabiki na watumizi wa mitandao ambao anasema tangu Jumatano wamekuwa wakimwambia kutia kichwa chake maji.

Faith kupitia Instagram yake aliweka wazi kuwa tangu mwanasosholaiti mwenzake Vwera Sidika kupasua mbarika kuwa aliamua kufanya upasuaji wa kurudisha umbo la makalio yake kiasili baada ya kupitia mateso, sasa walimwambia kuwa yeye ndiye anafuata mkondo huo hivi karibuni.

Lady Risper alisema ni kweli yeye alifanyiwa upasuaji wa kutunza mwili wake ila si ule wa kuongezewa makalio.

Alisema upasuaji alioufanyiwa ni aina ya Liposuction kwa lugha ya kimombo na wala hauhusiani na kuongeza makalio bali kupunguza ufuta mwilini na hauna madhara yoyote.

Aliwaambia wale wanamwambia kutia kichwa chake maji akisubiria matatizo kama yaliyompata Sidika kukoma kwani kama ni kumsubiri pia aseme amepitia maumivi, basi watasubiri sana.

“Na ndio nilifanyiwa liposuction ili kuondoa mafuta mengi tumboni baada ya kujifungua, sikuwahi kufanyiwa upasuaji kwenye makalio yangu... ni ukweli lakini naomba wale mnaingia DM yangu kuniambia kuwa mimi ndiye ninafuata mkondo mkome,” Lady Risper alisema.

Vera Sidika ndiye gumzo mitandaoni ndani na nje ya nchi baada ya kuweka wazi kuwa ilimbidi kufanyiwa upasuaji ii kuondoa makalio yake yenye umbo nene aliyokuwa ameyapata kutokana na upasuaji wa awali wa kuyaongeza.

Sidika aliwausia wanadada wenzake kuwa ni hatari sana na hata kuwashauri kukumbatia maumbile yao kwani upasuaji ule ulikuwa umemletea shida kwa muda mrefu mpaka kufikia hatua ya kufanya uamuzi wa kutafuta mwonekano wake wa kiasili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved