aliyekuwa muigizaji wa Tahidi High Omosh Kizangila ameweka wazi kuhusu madai yanayomhusisha na kusongwa kimawazo.
Akizungumza katika video ambayo alipakia kwenye YouTube yake, Kizangila alisema kwamba huo ni uongo kwani yeye yuko mzima wa afya na kiakili wala hasumbuliwi na tatizo lolote la unyongovu.
Omosh alisema kwamba huenda wale waliokuwa wanaeneza uvumi kuwa anakumbwa na msongo wa mawazo walimuona akiwa amekasirika na kudhani ana unyongovu.
Alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya mtu mwenye unyongovu na mtu mwenye hana furaha na kuwataka wanablogu kuacha kulitumia jina lake kama maudhui kwa ajili ya kupata ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.
“Wacheni hiyo stori, wanablogu bana wacheni kusema mimi niko na unyongovu, mimi ukiiangalia nakaa mtu ako na msongo wa mawazo? Kuna tofauti ya kutokuwa na furaha na kuwa na msongo wa mawazo. Nimekuwa bila furaha kwa wiki kadhaa kutokana na kupoteza rafiki zangu na jirani yangu pia,” Omosh alisema.
Pia alisema kuwa kitu kikubwa amabcho kimempata kwa mshangao mkubwa ni kusikia watu wakisema kwamba familai yake imemtoroka, jambo ambalo alilitaja kuwa porojo tu.
Aliwapa changamoto wale wanaosema kuwa familia imemtoroka kuenda nyumbani kwake na kuona kama kweli familia yake iko ama haiko.
“Mimi nataka kukuambia hivi, wewe enda tu nyumbani ukipata hiyo familia haiku kuja uniambie. Mimi kitu najua familia yangu iko nyumbani,” Omosh alisema.
Aliwaambia wale wanaosema kuwa amesongwa kimawazo kuenda kwenye mtandao wake wa Tiktok na kujionea jinsi anafanya sekeseke na mitikasi itakayowaonesha kwamba kweli hana msongo wa mawazo.
Wikendi iliyopita habari za muigizaji huyo kuwa na msongo wa mawazo zilipasua mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakimhurumia na wengine wakimsuta kwamba amesaidiwa mara nyingi wala hataki kujiongeza.
Mwanamuziki Akothee alimtaka Omosh kujitokeza wazi na kueleza wahisani wema kuhusu kile ambacho angetaka wamfanyie ile tatizo la unyongovu limuondokee kabisa.