Mwanamuziki Whozu amemsifia mpenzi wake ambaye ni mwigizaji, Wema Sepetu kwa picha yake ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram
Whozu alisema kuwa mapenzi yake na Sepetu hayawezi kufika tamati kama wanavyodhania wanamitandao na mashabiki wake.
Alidokeza kuwa yeye yuko kwenye mahusiano hayo na Sepetu na hataondoka wala kumwacha mpenzi wake hata kifanyike nini.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa yeye hana utatanishi wowote na kuwa ana utulivu mwingi haswa akiwa kwenye mhusiano.
"Ujanja sina ndugu zangu, nikiachwa hapa mje tu msibani," Whozu alisema na wakati huo huo akiashiria mapenzi ya dhati kwa Sepetu.
Sepetu alijibu kwenye picha hiyo na kusema kuwa yeye na Whozu hawana kikomo na kuwa pia yeye ako kwenye mahusino hayo na moyo wake wote.
Alisema kuwa bila Whozu maisha hayawezi kuenda sambamba na kuwa anafurahia kuwa mpenzi wake Whozu.
"Unadhani maisha bila wewe yatakuwa maisha tena? Haachwi mtu Chibaba," Sepetu alimjibu mpenzi wake.
Sepetu pia alichapisha picha na ujumbe kwenye mtandao wake na kuwasihi mashabiki wake kuukubali uhusiano wake na Whozu.
Alisema kuwa hana ubaya na mtu yeyote na kuwa waache kuyaingilia maisha yao kwa fujo na kutamka mambo ambayo hawana budi ila kukubali.
Zaidi ya hayo, mashabiki wake wamekuwa wakimkemea na kumlaumu Sepetu kwa kuwa na mwanamuziki huyo na pia hawajaonekana kuwa wenye furaha.
"Kama bado mna makasiriko, nawaonea huruma. Tukubali yaishe jamani. Mengine tunamuachia Mungu, ama vipi?" Sepetu aliwaamba mashabiki wake.
Mwigizaji huyo aliwaonyesha mashabiki wake upendo licha ya kufokewa na kutusiwa na kusema kuwa bado anawapenda .
Sepetu alisema kuwa watu waache kuombea mabaya uhusiano wake na Whozu na kuwa ni Mungu tu ndiye anayefahamu ya mbeleni na ana uwezo wa kumhukumu.
Aliapakia picha nyingine pia na kusema kuwa mapenzi yake na Whozu yamempa muonekano wa kumeremeta kwa jinsi anavyokaa.
"Mapenzi yananikalia vizuri jameni," Sepetu alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Alisema pia kuwa ana furaha kuwa mtu aliyezama kwenye mapenzi.