logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanasosholaiti Huddah Monroe akiri hayuko katika hali sawa

Huddah alimwomba Mungu ampatie hali ya utulivu na kumuondolea wasiwasi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 October 2022 - 12:46

Muhtasari


  • •Monroe, katika ujumbe ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram alidokeza kuwa hayuko sawa vile.
  • •Mwanasosholaiti huyo pia alisema kuwa anataka kuwa na ujasiri wa kutatua shida zozote zinazomkumba.

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewahimiza mashabiki wake kuangazia maombi ili waweze kuwa na mafanikio.

Monroe, katika ujumbe ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram alidokeza kuwa hayuko sawa vile.

Alimwomba Mungu ampatie hali ya utulivu na kumuondolea wasiwasi. Pia aliomba ukamilifu katika maisha yake.

Alisema kuwa hajakuwa sawa na kuwa amekuwa akipitia mengi ambayo hayajakuwa yakimpa amani.

"Mpendwa Mungu, Kwa muda saa nimekuwa nikijihisi kukosa uthabiti kwenye maisha yangu na nimekuwa nikihisi kutaka kufa moyo. Ninyooshee mkono wako wa neema na rehema," Monroe aliandika.

Mwanasosholaiti huyo pia alisema kuwa anataka kuwa na ujasiri wa kutatua shida zozote zinazomkumba.

Monroe aliongeza kuwa angetaka kuonyeshwa upendo wa Yesu ili aweze kutoka kwenye hali hiyo inayompa matata.

Alimwomba Mungu ampatie uwezo wa kutofikiria kinachosemwa huko nje na kuchukulia changamoto zozote zinazomkumba kwa njia chanya.

"Niwezeshe kuwa na akili ya utulivu kwenye mazingira yaliyotulia,nipe ujasiri uliomgumu ili niweze kuzipokea changamoto zozote zile. Nipe uwezo wa kujiamini ili niweze kujua kama umenielekeza kwenye njia hiyo na kuwa utanisaidia kuutimiza," alisema.

Alisema kuwa ombi lake ni la kutafuta amani ya moyoni na ya kimwili ili aweze kuzuia kuwa na msongo wa mawazo.

"Baba yangu mkubwa, endelea kunisaidia kunyamazisha kelele za nje. Nifunike kwa rehema yako, neema na unikinge na upendo wako usio na kifani," Monroe aliongeza.

Hii ni baada ya madai kuwa mwanasosholaiti huyo ni mjamzito kufuatia picha aliyopakia Instagram,  madai ambayo alijitokeza kukana na kusema umbo la tumbo lilisababishwa na nguo kubwa aliyokuwa amevaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved