logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sulwe, kitabu cha Lupita chenye simulizi ya msichana mweusi aliyechukia rangi ya ngozi yake

Kitabu hiki kina maudhui yenye nguvu, kitabu cha picha kinachogusa kuhusu rangi ya ngozi, kujistahi, na kujifunza kuwa urembo wa kweli hutoka ndani.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 October 2022 - 06:38

Muhtasari


  • • Sulwe ni msichana mweusi aliyetaka kubadilisha rangi ya ngozi yake ili kuwa kama wengine.
Mswada wa Sulwe kutoka kwa mwigizaji Lupita Nyong'o unafikisha miaka 3 tangu kuchapishwa

Wikendi iliyopita, mwigizaji na ambaye ni mshindi wa tuzo maarufu duniani za Oscars, Lupita Nyong’o alisherehekea miaka miatatu tangu kuchapishwa kwa kitabu chake cha kwanza – Sulwe.

Nyong’o ambaye ni mwigizaji mwenye makaazi yake nchini Mexico alijawa na furaha kuuona mswada wake huo kwa mara ya kwanza kwenye rafu za maduka ya kuza vitabu na kudokeza kwamba tangu kuchapishwa, ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kukiona kitabu chake kikiwa kimewekwa kwenye rafu za kuuza vitabu.

Kitabu cha Sulwe ambacho ni cha kuchekesha na maudhui yanayowalenga watoto ni simulizi moja na msichana mdogo wa Kiafrika ambaye ana mawazo ya kutaka kuibadilisha rangi ya ngozi yake ili kuwa kama ya mzungu.

Mswada huu wa Sulwe umekuwa ukishabikiwa sana duniani haswa na watu wenye rangi ya ngozi nyeusi ambao mara nyingi wanahisi kunyanyapaliwa na wenzao wazungu.

Kitabu hiki kina maudhui yenye nguvu, kitabu cha picha kinachogusa kuhusu rangi ya ngozi, kujistahi, na kujifunza kuwa urembo wa kweli hutoka ndani.

Kinasimulia kuhusu msichana mmoja kwa jina Sulwe ambaye anahisi kutokuwa na bahati kutokana na ngozi rangi ya usiku wa manane. Yeye ni mweusi kuliko kila mtu katika familia yake. Yeye ni mweusi kuliko mtu yeyote katika shule yake. Sulwe anataka tu kuwa mzuri na mkali, kama mama yake na dada yake. Lakini mwisho wa siku kitu kinamtokea na kubadilisha dhana yake kabisa kuhusu kuichukia rangi ya ngozi yake.

Katika kitabu hiki cha kustaajabisha cha picha, mwigizaji Lupita Nyong’o anatunga hadithi ya kuchekesha na ya kutia moyo ili kuwatia moyo watoto kuona urembo wao wa kipekee.

Katika kusherehekea miaka mitatau tangu kuchapishwa, Nyong’o alisema kuwa zaidi ya watoto elfu 60 watazawadiwa kitabu hicho katika taifa la Marekani.

“Heri ya miaka 3 ya Kuzaliwa, #Sulwe!!   💜✨ Hadi leo, ninajawa na shangwe kila wakati ninapoona kitabu kikiangaza kwenye rafu na mikononi mwa wasomaji wa thamani kote ulimwenguni! Kwa taarifa yenu, ndio mara ya kwanza nakiona kitabu change cha Sulwe kwenye makabrasha,” Lupita Nyong’o alisema kwa furaha.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved