Wanasema mtoto si nguo utaomba mtu na kila mzazi hufurahia ujio wa mwana na kusherehekea.
Hata hivyo kuna baadhi ya tamaduni ambazo kwa njia moja au nyingine hubagua watoto kulingana na jinsia zao na licha tamaduni hizi kupitwa na wakati baadhi ya jamii bado zinazikumbatia.
Shabiki mmoja wa mwanamziki Nameless aliibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kumwambia Staa huyo 'atafute mtoto wa kiume'.
Nameless alimjibu na kumwambia kwamba yeye na wengine walio na dhana potovu kama zake, nyakati zimebadilika na kila mtoto ana thamani yake ulimwenguni.
Watu wengi wameiga mkono kauli ya Nameless wakisema kuwa mtoto yeyote awe mvulana au msichana ana thamani sawa.
Zaidi ya hayo kujifungua watoto wa jinsia moja ni jambo la kawaida siku hizi na halifai kumkosesha yeyote usingizi.
Baadhi ya watu maarufu wamekuwa wakijifungua watoto wa jinsia moja bila utatanishi wowote wala kuonekana kuzingatia kutafuta mtoto wa jinsia nyingine.
Watu hawa maarufu wanaolea watoto wa jinsia moja ni kama:
Nameless na Wahu
Wanandoa wamebarikiwa na Mungu watoto maridadi wa kike. Siku chache zilizopita walifurahia kumpokea binti wao wa tatu na hata Nameless kujibandika jina la #babamabinti kuonyesha alivyofurahi kuwalea mabinti watatu.
Njugush na Celestine Ndinda
Hivi majuzi mkewe mcheshi Njugush alijifungua mtoto wa kiume na kuonyesha furaha yao kukaribisha mtoto mwingine wa kiume.
Alipotangaza kuwa amejifungua, Celestine Ndinda alijiita 'mama boys' kumaanisha mama ya watoto wa kiume.
Massawe Japanni
Mtangazaji huyu mahiri pia amebarikiwa na Mungu mabinti watatu na amekuwa akijivunia sana kuwalea mabinti wake warembo kupindukia.
Mwende Macharia
Mwanahabari huyu ni mama wa wavulana wawili na anajivunia kuwalea watoto wake wa kiume.