logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa awapachika ujauzito dada zake watatu, mama yao azirai baada ya kujua

Ripoti zinasema kuwa ndugu hao wanne walilelewa na wazazi wakali.

image
na Radio Jambo

Burudani18 October 2022 - 06:25

Muhtasari


•Dada hao watatu walipofikisha umri wa kutaka kujisimamia wanadaiwa kuanza kuwa na uhusiano wa karibu na kaka yao mara kwa mara.

•Mwishowe, dada wote watatu walipachikwa ujauzito na kaka huyo wao na baadaye wakajifungua.

Mkulima mmoja  amewashangaza wengi baada ya kubainia kuwa aliwapachika mimba dada wake watatu wa tumbo moja.

Ripoti zinasema kuwa ndugu hao wanne walilelewa na wazazi wakali na hawakuwa na uhuru mkubwa wa kutoka nje ama kujumuika na marafiki au majirani.

Dada hao watatu walipofikisha umri wa kutaka kujisimamia wanadaiwa kuanza kuwa na uhusiano wa karibu na kaka yao mara kwa mara bila wazazi wao kufahamu lolote hadi wakati walipopata mimba.

Wazazi hao ambao ni Wakristo walishtuka kwamba binti zao walikuwa wajawazito licha ya kuwa wakali kwao. Lakini walipouliza ni nani aliyehusika, jibu lao la kushangaza lilimfanya mama huyo azimie.

Ilibainika zaidi kijana  huyo alianza kulala na dada yake mzaliwa wa pili na baadae kuanza kuchumbiana na dadake mkubwa.

Dada wa mwisho pia ambaye alijua kilichokuwa kikiendelea pia alisisitiza kulala na nduguye na mwishowe mzaha mzaha ukatunga usaha.

Mwishowe, dada hao watatu walipachikwa ujauzito na kaka huyo wao na hatimaye wakajifungua vizuri.

Wazazi wao hawakuwa na lingine ila kukubali hali na kujilaumu kwa kuwa wakali na binti zao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved