logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diana Marua ashabikiwa jinsi anamuonesha mapenzi Morgan Bahati, mtoto wa kuasili

“Unakua unaenda???? @morgan_bahati 🤔 Nakupenda Mtoto wangu,” Diana Marua alimsifia.

image
na Davis Ojiambo

Burudani20 October 2022 - 06:31

Muhtasari


  • • Alisherehekewa kwa kuweka rekodi nzuri na kufutilia mbali dhana ya kuwa mama wa kambo sifa yao kuu ni kuwatesa watoto wasio wao.
Diana Bahatibamsherehekea mtoto wake wa kuasili, Morgan Bahati

Kwa mara nyingi kuna dhana potovu kwamba mama wa kambo sifa yake kuu ni kuwatesa watoto ambao hakuwazaa na ambao wako chini ya malezi yake.

Lakini kwa mtoto Morgan Bahati, mtoto wa kuasiliwa wa Msanii Bahati, mambo ni tofauti, kwani ana uhakika wa mapenzi kutoka kwa mamake wa kambo Diana Marua.

Kwa mara kadhaa, Diana Marua amekuwa akionesha upendo alio nao si tu kwa watoto wake wa kuwazaa bali pia hata kwa watoto wengine aliowapata na mumewe Bahati, kwa mfano mtoto wa mzazi mwenza wa Bahati, Yvetti Obura, Mueni pamoja pia na Morgan Bahati, mtoto ambaye Bahati alimtoa mitaani na kumuasili kama wake.

Diana Jumatano alipakia picha yake ya pamoja na mtoto Morgan kwenye Instagram yake na kummiminia sifa kwamba amekua kwa kasi ya ajabu jambo ambalo linamfanya kumuonea fahari kama mama ambaye amemkuza na kushuhudia kila hatua katika maisha ya mtoto huyo aliyeasiliwa kutoka mitaani.

“Unakua unaenda???? @morgan_bahati 🤔 Nakupenda Mtoto wangu,” Diana Marua alimsifia.

Wengi kwa mara kadhaa wamekuwa wakitaka kujua kama kweli mtoto huyo ni wa kuasiliwa na msanii Bahati au pengine ni wake ambaye alizaa na mwanamke mwingine asiyejulikana, wakitetea maswali yao kwamba Morgan kwa kiasi fulani ana mfanano na Bahati.

“Inashangaza jinsi watoto hawa hukua kwa haraka na hata kutupita urefu, lakini hebu ngoja, mbona anakaa kufanana na Bahati?” mtumizi mmoja wa Instagram aliuliza.

Ni juzi tu ambapo Diana Marua alitangaza jinsia ya mtoto wake wa tatu ambaye ni binti na mashabiki wake wanasubiria kwa hamu na ghamu kuzaliwa kwake na pengine kujuzwa jina lake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved