Mfanyabiashara Jamal Rohosafi amejikuta matatani na watumiaji wa mitandao baada ya kuandika ujumbe fulani kwenye Instagram yake akidokeza kwamba hana Imani kuna mwanamke ambaye hachepuki katika ndoa au uhusiano wa kimapenzi.
Katika chapisho hilo ambalo liliibua maoni kinzani, Jimal alionekana kuwasema wanawake wote kuwa ni michepuko na walupo na kusema kwamba kama hata mmoja ako ambaye hawezi kuchepuka katika uhusiano wake wa kimapenzi basi yeye hajawahi kutana na mwanamke wa sampuli hiyo.
“Samahani, nina mpenzi na siwezi kumsaliti, nampenda sana Je, wasichana wa aina hiyo bado wapo? Sababu sijakutana na mmoja ππ” Jimal aliandika kwenye Instagram.
Matamshi haya yake ambayo yalionekana kama kejeli kwa kina dada yalimweka kwenye tanuru na kutupiwa masimango ya kila rangi.
Wengine walimsuta vikali kwa kusema hivyo licha ya kujulikana wazi kwamba yeye ndiye alichangia ndoa yake kusambaratika na mkewe Amira, baada ya kumsaliti na mwanamitindo Amber Ray.
“Pia sijakutana na mwanaume anayeng'ang'ania kuwa ana mapenzi na mke wake na hawezi kumsalitiπππππ.....HEY amka kutoka usingizini na uende ukarekebishe familia yako,” mwanadada kwa jina Stephanie Yvonnie alimwambia.
“Vitu vingine maishani havionekani mara mbili, Mungu alikupa kimoja lakini umechanganyikiwa na moyo na hisia pia,” Myra Vine alimwambia akidokeza kwamba Jimal alipoteza bahati yake alipochanganyikiwa na hisia na kuchepuka.