logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gloria Muliro aadhimisha mwaka mmoja katika ndoa, amwandikia mumewe ujumbe mtamu

Rafiki, mume na mshirika wangu wa moshene - Muliro alimsifia.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 October 2022 - 10:25

Muhtasari


  • • Hapa ni kwako, hapa ni kwetu, hapa kuna miaka mingi ya furaha pamoja. Heri ya kumbukumbu ya miaka mpenzi! Nakupenda - Muliro.
Gloria Muliro na Evans Sabwami washerehekea mwaka mmoja katika ndoa

Mwimbaji wa nyimbo za injili Gloria Muliro na mume wake, mchungaji Evans Sabwami Jumapili walikuwa wanasherehekea mwaka mmoja tangu kufunga pingu za maisha.

Wawili hao walikula yamini ya kuwa mwili mmoja mnamo Oktoba mwaka jana katika hafla ya kipekee ya harusi iliyofanyika mjini New York, Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Muliro hakuweza kujizuia furaha yake na alimvisha koja la maua Sabwami kwa kumsherehekea kuamka kando na yeye kila siku kwa mwaka mmoja uliopita.

Muliro alimmtaja Sabwami kama rafiki wa kudumu aliyempata, pia akamtania kuwa mmoja wa mtu wa karibu sana ambaye wananong’onezeana udaku na umbea wote pasi na mipaka.

“Maadhimisho ya Furaha zaidi rafiki yangu mkubwa, mshirika wangu wa moshene, mume wangu. Upendo wako ni zawadi ambayo mimi hufungua kila siku. Hapa ni kwako, hapa ni kwetu, hapa kuna miaka mingi ya furaha pamoja. Heri ya kumbukumbu ya miaka mpenzi! Nakupenda 😘” Muliro aliandika.

Kabla ya kufunga harusi huko New York, wawili hao waliandaa hafla ya matayarisho ya harusi yao katika mji wa Eldoret mnamo Oktoba 8.

Muliro, mwimbaji wa nyimbo za injili aliyeshinda tuzo alimtambulisha mchumba wake na kuweka uhusiano huo hadharani mapema mwaka jana, baada ya kuwa singo kwa karibia miaka 6 kufuatia kuvunjika kwa uhusiano wake wa awali na mchungaji Omba.

Muliro aliondoka kwenye ndoa yake ya miaka 5 akimshutumu mume wa zamani kwa kukosa uaminifu, unyanyasaji wa kihisia, na usimamizi mbaya wa fedha zake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved