Mwanasiasa na mfuasi sugu wa Azimio Mahamed Alinur, kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa twitter amemuomboleza Rapa wa kikundi cha Amerika cha Migos, Takeoff.
Takeoff aliripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi.
Kulingana na ripoti za Amerika,rapa huyo alikuwa amemtembelea rafiki yake kwa likizo zilizokuwa kabla ya kupigwa risasi Billiard and Bowling huko Houston. .
Alikuwa na mjomba na mwanachama mwenza wa Migos, Offset pamoja na wasanii wa rapa wa Atlanta Young Thug na 21 Savage wakati kisa hicho kilipotokea.
Kundi hilo lilikuwa kwenye gari katika harakati zao kisha kuhudhuria sherehe ya rafiki yao Jas Prince kabla ya kuuliwa.
Kulingana na Hollywood Unlocked na wengine, Offset alidai kuwa gari lingine liliwazuia kuendelea na safari yao na kufyatua risasi.
Baadaye Takeoff alipelekwa katika hospitali kuu ya Georgia baada ya kuzirai na baadaye kutambulika kuwa amefariki.
"Siamini kwamba Takeoff kutoka kwa wana hip hop watatu wa Marekani Migos amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na kuuwawaMaombi yangu kwa familia yake, Quavo, Offset na Marafiki. lala salama Takeoff,"Aliandika Alinur.
I can't believe that Takeoff from the American hip hop trio Migos has passed away after he was shot and killed over a dice game in Houston. My prayers to his family, Quavo, Offset and Friends. RIP Takeoff.
— Alinur Mohamed (@AlinurMohamed_) November 1, 2022