Mwanavlogu Thee Pluto amedokeza kuwa mpenzi wake Felicity Shiru anatarajiwa kujifungua wakati wowote sasa.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Pluto alipakia picha yake na Felicity wakiwa hospitalini wakiijitayarisha kujifungua kwa mama huyo.
Alimwandikia mpenzi wake ujumbe mtamu huku akimshukuru kwa kuwa na ujasiri kwa wakati wote wa ujauzito wake.
“Wakati unadidimia. Wacha nianze kwa kusema kuwa kwangu wewe ni superhero. Mtu aliye na nguvu na upendo wangu kwako unakua kila siku. Umekuwa mrembo zaidi ya nyakati zote,” Pluto alisema.
Baba huyo mtarajiwa alieleza kuwa ana hofu za kuwa mzazi kwa mara ya kwanza ila ana imani kuwa yeye na mpenzi wake watakuwa na uhusiano wa karibu zaidi mtoto wao atakapozaliwa.
Hata hivyo Pluto alisema kuwa atafanya anachoweza ili mtoto na mpenzi wake wapate mahitaji yao na upendo kamili.
“Nina hofu kwa kinachokuja. Nina wasiwasi ya kuwa mtoto wetu hatanipenda ama kushindwa kutekeleza wajibu wangu vizuri, ya kuwa wanaweza kukukasirisha kisha kubadilisha mahaba ambayo tulikuwa nayo. Lakini wakati wowote ambao nina mawazo haya, nakuangalia tu kisha ninakumbuka jinsi ulivyotatua chochote ambacho kimekuwa kikikukwana wakati huu wa ujauzito,” mwanavlogu huyo alisema.
Alisema kuwa Felicity amekuwa chanzo cha utulivu na hofu yake kudidimia na anajua kuwa watakauwa sawa hata baada ya kujifungua.
“Kwa sababu hata kifanyike nini, huyu mtoto atakuwa na damu yako na damu yangu ila zaidi ya hayo nataka kuchukua fursa hii kusema hiki, asante sana mpenzi wangu,” alisema.
Mashabiki wao waliwatakia mema kwa hatua yao.