logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati atangaza mapenzi yasiyoisha kwa bintiye wa kwanza Mueni

Mueni alionekana kufurahi sana kuwa pamoja na baba yake, Bahati.

image
na Radio Jambo

Burudani09 November 2022 - 17:29

Muhtasari


  • Bahati ni baba  wa watoto watatu na Diana. Mtoto mdogo zaidi, Malaika, alizaliwa siku chache zilizopita

Mwanamuziki maarufu Bahati ametangaza kwamba atakuwepo kila wakati kwa binti yake wa kwanza Mueni.

Bahati pia alifichua mapenzi yake yasiyoisha kwa bintiye. Aliapa kwamba atakuwa tayari kumsaidia Mueni kila wakati.

Mueni ni binti ya Bahati na mpenzi wake wa zamani, Yvette. Walibarikiwa na mtoto lakini walitengana baada ya muda mfupi.

Mwimbaji huyo aliendelea na  kuoa mke wake wa sasa, Diana.

Bahati ni baba  wa watoto watatu na Diana. Mtoto mdogo zaidi, Malaika, alizaliwa siku chache zilizopita.

Wanandoa hao walifurahi kumkaribisha mtoto wao baada ya safari ya ujauzito yenye changamoto

Mueni alionekana kufurahi sana kuwa pamoja na baba yake, Bahati.

Walishikana mikono na kutabasamu kipindi hicho. Hii ilionyesha wazi kwamba wanafurahia mapenzi ya baba na binti Hakika wanapendana.

"Kwa Binti Yangu mzaliwa wa kwanza. Nitakuwa hapa kwa ajili yako kila wakati. Daima nitakuwa Shabiki wako Mkuu. Nakupenda kwa moyo wangu wote ❤,"Bahati Aliandika.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved