Felicity avunja kimya baada ya Andrew Kibe kuwauliza wafanye DNA

Aliendelea na kumshukuru mwanawe, kwa kumbadilisha na kufanya aitwe baba,na kupewa heshima.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram kwenye, kipindi cha maswali na majibu, mmoja wa mashabiki wake alimuuliza iwapo watafanya vile Kibe alikuwa amewauliza
Thee Pluto,Mwanawe na Felicity
Image: FELICITYINSTAGRAM

Muunda maudhui Felicity Shiru, amevunja kimya baada ya mtangazaji Andrew Kibe kuwauliza wafanye DNA ya mtoto wao na mpenzi wake Thee Pluto.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram kwenye, kipindi cha maswali na majibu, mmoja wa mashabiki wake alimuuliza iwapo watafanya vile Kibe alikuwa amewauliza.

"Kibe alisema mfanye DNA mtafanya kweli?"Shabiki aliuliza.

Huku akijibu swali hilo mama wa mtoto mmoja alisema kwamba hataki kuongea vibaya kutokana na usemi wake Kibe.

"Acha nisongee vibaya,"Alijibu Felicity.

Felicity alibarikiwa na mtoto wake  Zoey tarehe 4/11/2022.

Thee Pluto akisherehekea kuzaliwa kwa mwanawe alimnakili ujumbe wa kipekee,huku akimjulisha kwamba ametimiza ndoto yake.

Aliendelea na kumshukuru mwanawe, kwa kumbadilisha na kufanya aitwe baba,na kupewa heshima.

"Nimetimiza ndoto zangu kwa kumpata mwanangu. Karibu duniani mtoto wangu @zoey_pluto Umenibadilishia jina nikawa mzazi na ukanipa heshima. Nakuombea Maisha mema. My true love ❤️,"Aliandika Pluto.