Wingu la simanzi na majuto lilitanda kwenye mioyo ya wanafunzi wa kidato cha nne baada ya mmoja wao kuzikwa mnamo Novemba 14.
Mwanafunzi huyo alizikwa kaunti ya Kirinyanga huku wazazi na majirani wakionyesha huzuni yao kutokana na kifo cha msichana huyo mchanga.
Mwanafunzi huyo, Grace Wanjiku alifariki kwenye maporomoko ya maji kwenye mto wa Kathitha walipokuwa wamezuru mlima Kenya kwa ziara ya shule kama njia moja ya kujifurahisha kabla ya mtihani wao wa kidato cha nne kuanza.
Kwenye video ambayo ilipakuliwa kwenye mtandao ya Tiktok ulionyesha waombolezaji wakiwa wanahuzunika na wengi wakiwa wamefika kumpa mkono wa burini msichana huyo.
Kifo cha mwanafunzi huyo kinaendela kuzua hisia nzito kutoka kwa Wakenya kuhusiana na usalama wa wanafunzi wakiwa shuleni kwani wanaamini tukio hili lingeepukika na familia yake Grace haingeishi kwa majuto ya kumpoteza mwanao ambaye pengine angewasaidia kwenye siku za usoni.
Inahuzunisha sana ikionekana mwanafunzi huyo alifariki wiki tatu kabla ya kufanyika kwa mtihani wa kidato cha nne ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Hisia za kuhuzunisha ziliandikwa kwenye mtandao wa tiktok huku wanamitandao wakiungana na familia kutoa rambirambi zao na kuwaombea Mungu awape nguvu nyakati hizi za kupoteza mpendwa wao.
''Makiwa familia nzima. inasikitisha kumwona msichana huyo mchanga amekufa'' mmoja mtumizi wa mitandao aliandika.
''Mungu awafariji wazazi na wanafunzi wa Mugoiri. Mkasa huo hauwezi elezeka kwa maneno'' mwingne aliandika