Mnamo Novemba 21,2022, Mshambulizi wa Manchester United Cristiano Ronaldo alivunja rekodi ya dunia baada ya kufikisha nusu bilioni ya wafuasi kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Ameafikia hatua hii baaada ya kuvunja rekedi nyingine hivi majuzi ya picha yake akiwa na Lionel Messi kuvutia zaidi ya watu milioni 35.1 kwa siku moja, jambo ambalo lilizua gumzo katika ulimwengu wa soka, huku wengine wakitangaza kuwa ni picha bora zaidi ya michezo wakati wote.
Ronaldo kwa sasa ndiye mtu anayefuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii duniani.
Zaidi ya hayo nyota huyo wa Ureno amepata kuvuma sana kutokana na mahojiano ya kusisimua na mwanahabari Piers Morgan, mahojiano yaliyopaka matope hadhi ya Manchester United na pia kumchafulia jina meneja Erik ten Hag .
Huo ni uthibitisho wa mafanikio yao makubwa kupitia maisha ya soka ya hadithi ambayo wamejijengea kwa miaka 15 iliyopita.
Kikosi cha Man United kinalenga kumtimua Ronaldo kutokana na mahojiano hayo yalokuwa na utata.
Ronaldo, anatarajiwa kushiriki awamu ya tano ya Kombe la Dunia akiwa na Ureno mwezi huu.
Mpinzani wake wa muda mrefu Messi anasalia mtu wa pili kwa kufuatiliwa zaidi duniani.
Wanasoka hao mashuhuri wa kila wakati ndio majagina wa kabumbu pekee katika 10 bora ya watu wanaofuatiliwa zaidi kwenye Instagram.