Vera Sidika amsifia Sakaja baada ya kusema haya kuhusu muziki kwenye magari

Vera alijibu kwa kusema kuwa Sakaja ndiye gavana bora zaidi kuwahi kutokea.

Muhtasari
  • Kulingana na video Sakaja anadai kuwa madereva wanaruhusiwa kucheza muziki wenye sauti kubwa kwa magari yao na kwamba abiria wako huru kufanya hivyo
Vera Sidika
Image: Vera Sidika Instagram

Vera Sidika ni mmoja wa Watu Mashuhuri wa Kenya na pia mwanasosholaiti. Dakika chache zilizopitakupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia video ya Gavana wa Nairobi Jonhson Sakaja akizungumzia kuhusu Muziki wenye sauti kubwa kwenye magari ya uchukuzi wa umma.

Vera alijibu kwa kusema kuwa Sakaja ndiye gavana bora zaidi kuwahi kutokea.

"Best governor ever!!! so cool."

Kulingana na video Sakaja anadai kuwa madereva wanaruhusiwa kucheza muziki wenye sauti kubwa kwa magari yao na kwamba abiria wako huru kufanya hivyo.

Kwa Sakaja, suala la watu kulalamika kwa sauti kubwa lilikuwa ni historia.

"Na hii mambo kwenye graffiti na muziki wanasema ni mbaya, iyo ni ufala wa zamani sana. It is part of the culture. Kama mtu anataka matatu haina mziki angojee aingie yenye haina mziki na kama mtu anataka kusema iko na ngoma aingie yenye iko na ngoma. ," Sakaja alisema