Wake za nyota wa Mugithi Samidah Karen Nyamu na Edday Nderitu nusura waanze vita wakati wa onyesho lake la Mugiithi huko Dubai mnamo Desemba 16, 2022.
Onyesho la mwisho la Samidoh kabla hajarejea Kenya lilifanyika Ijumaa usiku huku makumi ya Wakenya wakihudhuria hafla hiyo iliyosheheni sana.
Drama ilianza Karen alipoenda moja kwa moja hadi pale Samidoh alikuwa ameketi na kukaa mapajani mwake kwa nguvu.
Edday, alisimama pale alipokuwa ameketi na kwenda na kumshika mkono mumewe hata wale walinzi walipojaribu kuwatenganisha wanawake hao wawili.
Video inayosambaa mtandaoni inawaonyesha Karen Nyamu na Samidoh wakiwa kwenye makabiliano.
Na dakika chache baadaye, inasemekana Karen alipoteza hisia zake na nusura ampige makofi Samidoh wakati walinzi wake walipoingilia kati.
Edday alisimama na kujaribu kumdaka Karen kutoka kwa mumewe kabla ya Karen kuchukuliwa na walinzi.
Kupitia kwenye ukurasa wa facebook wa Bernice, amemwandikia mkewe Samidoh ujumbe wa kutia moyo huku akimwambia kwamba yuko kwenye maombi yake, na kwamba anapaswa kumshika mumewe kwa nguvu.
Alimwambia wakati mambo yanapokuwa mazuri ni wakati shetani anakuja na kwamba yeye ndiye mwenye taji anapaswa kurekebisha vizuri kwani siku bora zinakuja.
Alimwambia Karen Nyamu ambaye ni side chick kwa Samidoh kujua daima anakumbuka msimamo wake.
"Edday nderitu uko kwenye maombi yangu pole mpenzi ndege yangu ilikatizwa uswizi lakini mshikilie mume wako kwwa nguvu,kumbuka mambo yanapokuwa mazuri ndio shetani anakuja , tulia na ujue hili litapita kumbuka wewe ndio uko na taji đź‘‘rekebisha vyema kumbuka siku njema zaja Samidoh Leo umecheza kama wewe.... thank you soo much the security was on point sidechic always remember your position wacha kusumbua watu aah nkt ..."