Ivy Namu, mke wa mzalishaji wa kipindi cha 10over10 kwenye runinga ya Citizen, Willis Raburu hatimaye ameasi chama cha wenye rasta baada ya kunyoa rasta zake ambazo alikuwa amezilea kwa miaka mitano iliyopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Namu alisema kuwa alikuwa anataka kuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 kwa njia mpya bila kuwa na muonekano wake ambao kwa miaka 5 wengi wamekuwa wakiujua kama nembo ya utambulisho wake.
Kinyume na wengi wanaosema kulea rasta ni lele mama, Namu alidokeza kuwa amepitia mengi kuhakikisha kuwa rasta zake zilikuwa katika hali nzuri na kufichua kuwa ameshajitambua na alikuwa anataka mwanzo mpya kwa mwaka mpya.
“Rasta zangu zimenipitia mengi, wakati ambao nilihisi kama kujipata ni suala la kuishi. Nimekua sana tangu wakati huo na nimebarikiwa vya kutosha kutazama maombi yangu yakidhihirishwa katika ukweli; Niko na raha na tayari kwa enzi mpya katika maisha yangu,” Ivy Namu alisema.
Lakini pia alitaka mashabiki wake kuweka alama kama muonekano wake bila rasta ulikuwa wa kweli ama aliotea huku akisema kuwa mtu si lazima uwe na nywele hizo ili kubaki katika chama cha machokodindo.
Mashabiki wake walimsifia kwa muonekano mpya huku shabiki wake mkuu ambaye ni mume wake Raburu akimhongera kwa kubadilisha muonekano mzuri.
“Eish! Yawa kipande cha mbinguni, kipande cha cosmos, mkusanyiko wa nyota zilizokusanyika katika uso mmoja. Uzuri kama huo. Nakupenda na kukupenda,” Raburu hakuweza kujizuia.
“Aaaaahhh furaha na hisia nywele ... Na bado hang up juu ya wewe hatimaye alifanya hivyo 😂😂. Unaonekana dope AF karibu kwa chama cha nywele za shati,” mtangazaji Aniitah Raey alisema.
Kunyoa kwa Ivy Namu rasta zake kunakuja miezi kadhaa baada ya mumewe Willis Raburu pia kunyoa zake.