Mwanamuziki wa Dancehall KRG the Don ametoa ‘rate card’ yake kwa wale ambao wanataka awafuate kwenye mitandao ya kijamii.
Kulingana na KRG, huwa hamfuati mtu yeyote haswa kwenye ukurasa wake wa Instagram na sasa kama mtu yeyote anataka Msanii huyo amfollow kwenye mitandao ya kijamii ni sharti azame mfukoni na kutengana na kiasi cha shilingi laki mbili na nusu za Kenya kwa ajili ya hilo.
Msanii huyo alisema alichukizwa na mwanaume fulani ambaye hamjui na alimtaka kumfuata kwenye mitandao kisa tu kujikuta ameketi karibu na yeye katika sehemu moja ya starehe.
“Mtu tu nisiyemjua aliniamia nimfuate kwenye mtandao kwa sababu tu alijipata ameketi karibu na mimi nikijivinjari, halafu meneja wangu akamuuliza yeye ni mtoto wa nani, akasema ni shabiki wa KRG.Mimi huwa sifuati mtu yeyote mitandaoni, kama sikujui kibinafsi au hauna kakitu. Lakini ukifika bei ya dola elfu mbili (Ksh 247K) nitakufollow. Bughaa ako na mzio kwa utiaji na umaskini,” KRG alijipiga kifua.
Msanii huyo ambaye kwa mara kadhaa amekuwa akinukuliwa kujigamba kuwa ni tajiri bilionea mwenye mali nyingi alisema kuwa hawezi mtambua mtu yeyote awe ni shabiki au la ambaye hana kitu.
Kulingana na yeye, pesa ndio kila kitu.
KRG amewahi sema kuwa utajiri wake ni bilioni 5, jambo ambalo mpaka sasa wengi hawajawahi kubaliana naye, wengine wakisema hata hawajui wimbo wake hata mmoja na hivyo kuhoji uhalali wa utajiri huo wake.