"Namficha kama bangi" Ex wa Mulamwah, Carrol Sonnie azungumza kuhusu mahusiano yake mapya

Sonnie amesema hayuko tayari kumtambulisha mpenzi wake mpya kwa umma.

Muhtasari

•Mama huyo wa binti mmoja hata hivyo ameweka wazi kwamba hayuko tayari kumtambulisha mpenzi wake mpya kwa umma.

•"Huyu siwezi waonyesha," Sonnie alijibu.

Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Ni dhahiri kwamba mpenzi wa zamani wa mchekeshaji Mulamwah Caroline Muthoni, almaarufu Carrol Sonnie tayari ameshasonga mbele na maisha yake. 

Sonnie na Mulamwah walitangaza kuvunjika kwa uhusiano wao mwezi Oktoba 2021, wiki chache tu baada ya kumkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja. Sasa inaonekana kwamba muigizaji huyo tayari amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba mazito na mwanamume mwingine ambaye bado hajamtambulisha hadharani.

Mama huyo wa binti mmoja hata hivyo ameweka wazi kwamba hayuko tayari kumtambulisha mpenzi wake mpya kwa umma.

"Huyu namficha kama bangi," alisema kwenye Instastori zake.

Sonnie alikuwa akimjibu shabiki wake mmoja ambaye aliuliza kuhusu wakati ambapo anapanga  kuonyesha aliyeridhi Mulamwah.

"Mwanaume mpya ni nani? Aki si utatuamsha vidonda vya tumbo," shabiki mwingine aliuliza kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Shabiki huyo huenda alichochewa kuuliza kutokana na jinsi muigizaji huyo amekuwa akizungumzia mapenzi yake mapya.

"Huyu siwezi waonyesha," Sonnie alijibu.

Uamuzi wa muigizaji huyo wa kumficha mpenzi wake ili asichunguzwe na umma unaeleweka kwa kuzingatia yote yale ambayo alilazimika kupitia wakati wa kutengana na mzazi mwezake Mulamwah na drama zilizojitokeza baadae.

Takriban miezi mitano iliyopita, Mulamwah alimuonya mpenzi huyo wake wa zamani dhidi ya kuruhusu mahusiano yake mapya kutatiza uhusiano wake na binti yao Keilah Oyando.

Mchekeshaji huyo alimtaka mzazi huyo mwenzake kudumisha heshima hata baada ya kujitosa kwenye mahusiano mengine.

"Kuwa na heshima, chumbiana na mtu yeyote unayetaka, bora uwaweke mbali na njia ya msichana huyo mdogo na yangu!" Mulamwah alimwandikia mpenziwe wa zamani kupitia  Instagram.

Mulamwah pia alimshtumu muigizaji huyo kwa kuchumbiana na mzee wa miaka 60 aliye kwenye ndoa nyingine tayari.

Alichapisha picha kadhaa za mpenzi huyo wake wa zamani na kutoa maelezo ya kuyapa nguvu madai yake.

"Mnak*lan* na wazee wa miaka 60 halafu mnakuja kuset standards kwa mtandao na picha za kipuzi na mahojiano ya kupuzi,"

Baadae aliibua madai kuwa 'mzee' ambaye mzazi  huyo mwenzake anachumbiana naye anatishia maisha yake. 

Sonnie hata hivyo alijitokeza kupuuzilia mbali madai ya na kueleza kwamba mwanaume ambaye mpenzi huyo wake wa zamani  alikuwa akidai ni mpenzi wake mpya alikuwa ni mhubiri ambaye alitazamiwa kuwapatanisha.

Sonnie alidokeza kwamba yuko kwenye mahusiano mapya mwezi Julai mwaka jana ambapo alionyesha sehemu ya mwili wa mwanaume anayechumbiana naye. Hata hivyo hakuonyesha sura ya mpenziwe mpya.