Babu Tale atunukiwa Shahada ya Uzamivu kwa jukumu katika ujenzi wa taifa

Tale aliwashukuru wapiga kura wake kwa mchango mkubwa katika mafanikio yake.

Muhtasari

•Tale alisema alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu wa Falsafa kutokana na mchango wake katika uongozi.

•“Naishukuru nchi yangu kwa kuweka mazingira rafiki ambayo yametuwezesha kutambulika ndani na nje ya nchi." alisema.

Image: INSTAGRAM// BABU TALE

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale ametunukiwa shahada ya Uzamivu ya heshima na Chuo Kikuu cha Amerika.

Tale alisema alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu wa Falsafa kutokana na mchango wake katika uongozi.

"Leo ni siku ambayo siwezi kulinganisha na nyingine yoyote," aliandika kwenye Instagram.

“Naishukuru nchi yangu kwa kuweka mazingira rafiki ambayo yametuwezesha kutambulika ndani na nje ya nchi.

Babu Tale ambaye pia ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, alizidi kuwashukuru wapiga kura wake kwa mchango mkubwa katika mafanikio yake.

“Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, mmekuwa daraja la mafanikio yangu na niwashukuru kwa heshima ninayopewa sasa na yatakayonipata mbeleni, Mungu awabariki wote na ninaahidi kuwatumikia kwa bidii zaidi," alisema.

Mwaka 2020, Babu Tale alikua mpeperusha bendera wa CCM katika kiti cha ubunge baada ya kumshinda Waziri Msaidizi wa Kilimo wa Tanzania, Omary Mgumbe, ambaye alikuwa anashikilia nafasi hiyo.

Aliapa kuwa kiongozi mtumishi na kuishi kulingana na maadili ya ofisi na kutekeleza ahadi ambazo walitoa pamoja.