Harmonize afunguka kwa nini hajafuta tattoo ya Kajala licha ya kutengana

Mwimbaji huyo ameweka wazi kuwa yuko single na tayari kuchumbiana tena.

Muhtasari

•Harmonize alikiri kwamba, pamoja na mambo mengine mengi, yeye ni shabiki mkubwa wa wanawake wa Kenya.

• "Tatoo ni suala la kibinafsi. Sidhani kama ni kitu unaweza kuzungumza kuhusu.Tuangalie tu kama itakuwepo," alisema

Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Mwimbaji wa Bongo Rajab Abdul Kahali  almaarufu Harmonize yupo nchini Kenya alifanya show kubwa katika mji wa Embu siku ya Jumamosi jioni.

Wakati alipotua nchini bosi huyo wa Kondegang alifanya mazungumzo na Waandishi wa Habari ambapo alikiri mapenzi yake makubwa kwa Kenya.

Alikiri kwamba, pamoja na mambo mengine mengi, yeye ni shabiki mkubwa wa wanawake wa Kenya.

"Napenda mengi, kama wanawake warembo, hasa kwa kuwa niko single," alimwambia  Mungai Eve.

Staa huyo wa Bongo alidokeza kwamba yuko tayari kujaribu mahusiano na mwanadada kutoka Kenya baada ya kutemwa na Kajala.

"Niko tayari kujaribu. Nataka tu kuzama kwenye mahaba," alisema.

Takriban mwezi mmoja unusu, muigizaji Fridah Kajala Masanja alitangaza kuvunjika kwa mahusiano ya miezi kadhaa na mwimbaji huyo.

Ingawa hakuweka wazi kilichowatenganisha, Kajala alibainisha kuwa tayari amemsamehe Harmonize kwa kilichotokea.

Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema mwezi Desemba.

Wawili hao walionekana wenye furaha na mahaba sana katika takriban miezi saba ambayo walichumbiana kabla ya mahusiano yao kufika kikomo Desemba. Walikuwa wamerudiana Mei baada ya Harmonize kuomba msamaha.

Wakati akiomba msamaha na kumsihi Kajala amrudie, Harmonize alipiga hatua kubwa ya kuchorwa tattoo ya picha ya kumbukumbu ya muigizaji huyo akiwa na binti yake Paula Paul kwenye mguu wake.Alipiga hatua hiyo kama mojawapo ya njia ya kumtongoza Kajala ili warudiane  baada ya kuwa wamekosana kwa mwaka.

Hata baada ya kutengana mwishoni mwa mwaka jana, mwimbaji huyo bado amehifadhi tattoo hiyo. 

Konde Boy alipoulizwa kwa nini bado hajachukua hatua ya kufuta picha hiyo, alisema, "Tatoo ni suala la kibinafsi. Sidhani kama ni kitu unaweza kuzungumza kuhusu.Tuangalie tu kama itakuwepo,"

Wakati wa mahusiano yao, Harmonize na Kajala pia walichorwa tattoo za herufi ya kwanza ya majina yao kwenye vidole.