logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Esther Musila azungumzia kurudiana na mumewe Guardian Angel baada ya kutoka nje ya ndoa

Bi Musila alibainisha kwamba hawezi kuishi bila maji, chakula na mume wake.

image
na Samuel Maina

Burudani08 February 2023 - 10:16

Muhtasari


  • •Shabiki alitaka kujua ikiwa anaweza kurudiana na mume wake baada ya kukanyaga nje ya ndoa.
  • •Alijibu, "Wow, ndiyo na hapana, lakini  itategemea."

Mke wa mwimbaji Guardian Angel aliwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram.

Katika kipindi hicho wanamitandao walimuuliza maswali mengi kuhusu maisha yake, familia yake, ndoa, kazi na mambo mengine.

Mtumiaji mmoja wa Instagram alitaka kujua ikiwa anaweza kurudiana na mume wake baada ya kukanyaga nje ya ndoa.

"Je, unaweza kurudi kwa mpenzi wako kama alitoka nje ya ndoa," shabiki aliuliza.

Alijibu, "Wow, ndiyo na hapana, lakini  itategemea."

Katika kipindi hicho cha Q&A, mama huyo wa watoto watatu wakubwa pia alilazimika kujibu kuhusu iwapo anapanga kupata mtoto pamoja na mume wake Guardian Angel.

Je, Unapanga kupata mimba?" shabiki mmoja alimuuliza.

Musila ambaye alionekana kukerwa na swali aliloulizwa alijibu, "Je, hiyo inaongezaje thamani ya maisha yako??"

Pia alijibu vivyo hivyo wakati mtu mwingine kwa Instagram alipotaka yeye na Guardian walete mtoto wao duniani.

Kwa sasa Bi Musila ana watoto watatu wakubwa, wawili wa kiume na msichana mmoja. 

Wakati huo huo, Bi Musila alibainisha kwamba hawezi kuishi bila maji, chakula na mume wake.

Musila ,53, na Guardian Angel ,33, walifunga pingu za maisha mapema mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa takriban mwaka mmoja. Wawili hao wamekuwa wakifurahia ndoa yao na  kushiriki nyakati nzuri za mahusiano yao kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo, Bi Musila alibainisha kwamba hawezi kuishi bila maji, chakula na mume wake.

Hivi majuzi, Guardian Angel alimhakikishia mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kwamba hana majuto yoyote kwa kuamua kushiriki maisha naye huku akisema kuwa anaweza kufanya hivyo tena na tena.

"Peter Omwaka, ningeolewa nawe tena," aliandika kwenye picha ya kumbukumbu ya harusi yao inayoonyesha wakiwa wamekumbatiana.

Katika jibu lake kwa mke wake, Guardian Angel alisema, "Kukupenda ni maisha yangu Malkia wangu"

Mwimbaji huyo pia alichapisha picha yake na mkewe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na emoji za moyo zinazoashiria mapenzi.

"Mpenzi wangu," Musila alijibu chini ya picha hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved