Massawe Japanni amkaribisha bintiye kwenye ujana kwa njia maalum

Soraya, ambaye ni mtoto wa pili wa mtangazaji huyo anatimiza miaka 13.

Muhtasari

•Huku akimsherehekea bintiye, Massawe alimtakia neema ya Mungu maishani na kuomba ndoto zake ziweze kutimia.

•Massawe alimtaja Soraya kama msichana mdogo wa ajabu na kusema kuwa amekusudiwa kwa mambo makubwa.

Massawe Japanni na bintiye Soraya
Image: INSTAGRAM

Bintiye mtangazaji wa kipindi cha Bustani la Massawe kwenye Radio Jambo, Massawe Jappani anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi leo, Machi 8.

Soraya, ambaye ni mtoto wa pili wa mtangazaji huyo mahiri anaingia katika maisha ya ujana leo huku akitimiza miaka 13. 

Huku akimsherehekea bintiye, Massawe alimtakia neema ya Mungu maishani na kuomba ndoto zake ziweze kutimia.

"Binti yangu Soraya, barabara iliyo mbele yako ijazwe na mwanga. Bwana akulinde, na atimize ndoto zako. Mungu akusaidie utimize malengo yako," Massawe alimwandikia binti yake kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Hongera kwa mwanzo wa safari yako ya ujana! Heri ya siku ya kuzaliwa ya kumi na tatu binti yangu. Wewe ni maalum kila wakati ❤️ mama,"

Malkia huyo wa Swahili Radio alimtaja Soraya kama msichana mdogo wa ajabu na kusema kuwa amekusudiwa kwa mambo makubwa.

"Heri ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake mtoto wangu! Umekusudiwa kwa mambo makubwa," Massawe aliandika.

Mtangazaji huyo mwenye sauti ya kupendeza kweli aliambatanisha ujumbe huo na picha kadhaa nzuri za binti huyo wake wa pili.

Massawe ni mama mwenye fahari wa mabinti watatu warembo na mara nyingi amekuwa akionyesha jinsi anavyojivunia kuwalea.