logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wema Sepetu afunguka kutambulishwa kwa wakwe zake, kuwa pweke muda mrefu

Wema amedokeza kwamba mpenzi wake , Whozu tayari amemtambulisha kwa familia yake.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri10 March 2023 - 04:51

Muhtasari


•Muigizaji Wema Sepetu amedokeza kwamba mpenzi wake , Whozu tayari amemtambulisha kwa familia yake.

•Wema na Whozu waliweka mahusiano yao wazi mwaka jana baada ya kuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu.

Muigizaji mkongwe wa filamu Bongo, Wema Sepetu amedokeza kwamba mpenzi wake , Whozu tayari amemtambulisha kwa familia yake.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, Bi Tanzania huyo wa zamani alitakiwa kujibu kuhusu wakati atatambulishwa kwa wakwe zake.

"Kwani unadhani kwao hawanijui?" alijibu.

Mpenzi huyo wa zamani wa bosi wa WCB, Diamond Platnumz alibainisha kwamba mahusiano yake na Whozu yamemletea raha sana.

Wema alisema kwamba sasa yuko katika hali bora zaidi kwani kwa muda mrefu amekuwa pweke, jambo ambalo limemnyima furaha. 

"Mimi ni mtu napenda sana kuonyesha hisia zangu. Mimi ni wazi. Nikipenda napenda, nikichukia nachukia. Siwezi kujifanya. Nadhani kwa muda mrefu nimekuwa sijapenda na sijakuwa na furaha," alisema.

Wema na Whozu waliweka mahusiano yao wazi mwaka jana baada ya kuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu.

Mnamo siku ya Wapendanao, Wema alifichua kuwa mpenzi huyo wake ndiye sababu ya furaha kubwa aliyo nayo siku za hivi majuzi.

"Mkumbato wangu shweet, mpenzi wangu wa kukumbatia, sababu ya tabasamu langu lisiloisha❤❤❤,"  muigizaji huyo alimwandikia Whozu kwenye mtandao wa Instagram na kuambatanisha na picha yake.

Mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Diamond Platnumz aliendelea kumuita mpenziwe maneno matamu ya mahaba kama vile; Valentine's wangu, Furaha yangu ya kweli, Wangu wa pekee, Faraja yangu, Chaguo langu, Msiri wangu, Mshunu Wangu, miongoni mwa majina mengine mengi.

"Naapa mbele ya Mungu nakupenda sana Chibaba wangu Wallahy," alisema.

Whozu kwa upande wake alitumia siku ya Wapendanao kueleza baadhi ya sababu za kumpenda Miss Tanzania huyo wa zamani.

Mwimbaji huyo alidokeza kuwa mahusiano yake na Wema Sepetu yanahusisha upendo, heshima, amani na kujaliana.

"Mapenzi yanaweza kuwa mazuri sana kama utampata anaekupenda, kukuheshimu na kukujali. Asante mungu kwa kuniweka sehemu tulivu, Nisiwe Muongo Napata Amani ya moyo napata Furaha, Natabasamu naenjoy mapenzi yangu..😊🙏🏽

Nimetosheka sana na Chimama Wangu. Acha tu nikupende siku zote nibaki na wewe milele My Valentine❤️," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved