Marekani yatishia kuipiga marufuku TikTok iwapo haitauzwa – ripoti

Marekani inasema TikTok lazima iuzwe la sivyo ikabiliwe na uwezekano wa kupigwa marufuku nchini humo

Muhtasari

•Programu hiyo inashutumiwa kwa kusababisha hatari ya usalam wa taifa kwa kukusanya data kutoka data za mamilioni ya watumiaji.

Image: BBC

Serikali ya Marekani inasema TikTok lazima iuzwe la sivyo ikabiliwe na uwezekano wa kupigwa marufuku nchini humo, kwa mujibu wa ripoti.

Programu (app) hiyo ya kushirikisha video, inayomilikiwa na kampuni ya Kichina Byte Dance, inashutumiwa kwa kusababisha hatari ya usalam wa taifa kwa kukusanya data kutoka data za mamilioni ya watumiaji.

Ombi la kubadili umiliki, kwa mara ya kwanza liliripotiwa katika jarida la Wall Street Journal (WSJ), lilithibitishwa kwa BBC na TikTok.

Kampuni hiyo inasema mauzo ya kulazimishwa hayatabadili usambaaji wa data au upatikanaji wa programu ya TikTok.

Ikulu ya White House bado haijajibu ombi la BBC News la kutaka kauli yake.

Kwa miaka maafisa wa Marekani wamekuwa wakielezea hofu zai kwamba taarifa(data) kutoka kwa app hiyo maarufu zinaweza kuangukia mikononi mwa serikali ya Uchina.