logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mke wa Christian Atsu aondoka Ghana na watoto wote siku 3 baada ya kumzika mumewe

Claire kabla ya kuondoka alilitembelea kaburi la mume wake na kutoa buriani ya mwisho.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 March 2023 - 10:28

Muhtasari


  • • “Asante Ghana, hadi tutakapokutana tena, Christian Tunakupenda,” Claire aliandika kwenye Instagram yake.
  • • Claire, familia yake na watoto walikuwa nchini Ghana siku ya Ijumaa tarehe 17 Machi kwa maziko ya mwanasoka huyo wa Ghana.
  • • Ziara ya kihisia ya familia kwenye kaburi la Atsu ilikuwa fursa kwao kutoa heshima zao za mwisho kwa mume na baba yao wapendwa.
Mke wa Atsu akizidiwa na hisia wakati wa kuaga kaburi la mumewe

Claire, mke wa marehemu mwanasoka wa Ghana Christian Atsu ameondoka nchini Ghana siku tatu tu baada ya kumaliza shughuli ya kumzika aliyekuwa mumewe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Claire alipakia picha za majonzi akimpa buriani za mwisho mumewe Atsu na kuwaandikia wananchi wa Ghana ujumbe wa kwaheri, akisema kwamba Mungu akipenda wataonana tena siku moja.

“Asante Ghana, hadi tutakapokutana tena, Christian Tunakupenda,” Claire aliandika kwenye picha hizo.

Claire, familia yake na watoto walikuwa nchini Ghana siku ya Ijumaa tarehe 17 Machi kwa maziko ya mwanasoka huyo wa Ghana.

Wakati huo huo, iliripotiwa mapema kwamba, mke wa marehemu Christian Atsu na watoto walitembelea kaburi lake mara ya mwisho kabla ya kurejea Ulaya. Atsu, mwanasoka mwenye kipawa, aliaga dunia kwa huzuni wakati wa tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki.

Tetemeko la ardhi lilisababisha vifo vingi, ikiwa ni pamoja na Atsu, ambaye alizikwa katika mji wake wa Ada mnamo Machi 17, 2023.

Ziara ya kihisia ya familia kwenye kaburi la Atsu ilikuwa fursa kwao kutoa heshima zao za mwisho kwa mume na baba yao wapendwa.

Mke na watoto wake walikuwa wamefadhaika sana, na uchungu wa kufiwa ulionekana wazi katika machozi yao na maneno yao ya huzuni. Ziara hiyo ilikuwa fupi, lakini iliwaruhusu kupata muda wa kuwaaga kabla ya kurudi Ureno.

Atsu alikuwa mwanasoka mashuhuri ambaye alichezea vilabu mbali mbali, vikiwemo Chelsea, Everton, na Newcastle United. Pia alikuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya Ghana, ambapo alijulikana kwa kasi yake, wepesi, na ustadi uwanjani.

Baadhi ya wanamitandao walihisi kwamba mwanamke huyo anakwenda kinyume na mila na tamaduni za Kiafrika kwani mjane hafai kuondoka katika boma lake baada ya maziko, hadi angalau kwa siku 40.

Awali tuliripoti kwamba baadhi ya wanamitandao walizua wasiwasi wao na watoto wa Atsu kwa kusema kwamba hakuna hata mmoja aliyekuwa anamfanana kwa sura au rangi ya ngozi, huku wakihisi kwamba ni heri angeo mwanamke wa Kiafrika.

 

Kifo chake kilikuwa mshtuko kwa ulimwengu wa kandanda, na heshima zilimiminika kutoka kwa mashabiki na wachezaji wenzake kote ulimwenguni. Urithi wa Atsu kama mwanasoka mwenye kipawa na mwanafamilia mwenye upendo bila shaka utakumbukwa na wote waliomfahamu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved