Mchekeshaji maarufu nchini MCA Tricky hatimaye amejitokeza wazi kufichua sababu, kwa nini hakuhudhuria harusi ya Akothee.
Tricky alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliotarajiwa kujitokeza kwenye harusi hiyo, lakini cha kushangaza, mchekeshaji huyo hakuonekana popote Akothee alipokuwa akifunga pingu za maisha na mumewe.
Akizungumza kwenye mahojiano na 2mbili tv, MCA Tricky ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa Rue Baby, alisema kuwa sababu kubwa iliyomfanya asijitokeze kwenye harusi ya wakwe zake, ni kwa sababu yuko kwenye orodha ya watu watakaokwenda Uswizi. .
Tricky alisema kuwa hakuona sababu ya kuhudhuria harusi hiyo, kwa sababu ni miongoni mwa waliochaguliwa ambao watakuwa na Akothee nchini Uswizi.
Aliwataka watu kuacha kuwaza kupita kiasi, kwa sababu alikuwa na nafasi ya kujitokeza, lakini walikubaliana kwa pamoja na Akothee kuwa ataenda kwa harusi ijayo.
Mchekeshaji huyo alisema kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya harusi ya Julai 10, na hatawakatisha tamaa Wakenya, atajitokeza akiwa amepambwa vyema na atawawakilisha vyema huko nje.
Akuzungumza kuhusu uhusiano wake na Rue Baby, kwa ujumla alisema kwamba yeye na Akothee wana uhusiano mzuri, na ilikuwa ni mapenzi yake tu kutohudhuria harusi ya Kenya, bali kuhudhuria ile ya Uswizi.