Mwanasosholaiti maarufu Vera Sidika hamfuati tena mumewe, Brown Mauzo kwenye akaunti yake ya Instagram.
Vera aliondoa jina 'mke' kwenye maelezo yake ya Instagram. Jambo hili limezua gumzo miongoni mwa mashabiki wao huku wengi wakishuku kuwa uhusiano wao unayumbayumba .
Hili linajiri wiki chache baada ya Brown Mauzo kuacha kumfuata Vera Sidika kwenye Instagram na hata kuzifuta picha za Sidika kwenye ukurasa wake. Hata hivyo Mauzo bado anafuatilia mtoto wao Asia Brown.
Mauzo ni mwanamuziki na wawili hao walianza kuchumbiana mwaka wa 2020 walipokutana Mombasa. Wana mtoto mmoja pamoja, Asia Brown, aliyezaliwa mwaka uliopita huku wakimtarajia mtoto wao wa pili atakayezaliwa hivi karibuni.
Hapo awali, Vera Sidika aliwajibu mashabiki waliozua maswali ya iwapo wawili hao wameoana kihalali. Vera alisema kuwa alifunga ndoa kihalali na mume wake Brown Mauzo ila bado hawajafanya sherehe.
"Tumeoana kisheria ila hatujafanya harusi yetu,nawaahidi kuwa itakuwa karamu kubwa zaidi Afrika," aliandika Sidika.
Sidika mara si haba ametetea mumewe kila wakati mashabiki walipouliza maswali ya kipi anachofanya kando na muziki ili apate pesa. Sidika alisema kuwa mume wake ni mfanyibiashara asiyependa kuonyesha mali yake kwa umma.
Kando na hayo, Sidika aliwasuta mashabiki waliodai kuwa yeye ndiye anamfadhili mume wake kifedha.
Hata hivo si wazi kama wawili hao wamewachana na labda wanatafuta kiki kama ilivo ada , mwaka uliopita ,Vera Sidika alidai kuwa alienda kufanyiwa upasuaji kuondoa sehemu ya makalio yake akidai kuwa ilimletea shida za kiafya liliofanya wengi kuamini jambo hilo. Siku chache badaye ilidhihirika Sidika alikuwa anatafuta kiki ili kutoa kibao .