logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alikiba alianza kuimba akiwa na umri wa siku 7 tu! - mamake afichua

Akiwa na miaka mitatu alikuwa anacheza densi kwenye shughuli za harusi.

image
na Radio Jambo

Habari27 April 2023 - 06:10

Muhtasari


• Aidha mama huyo alifichua sababu ya kutokuwa mzungumzaji sana kwenye vyombo vya habari kuhusu maisha yake na wanawe.

• “Kila kitu kipewe nafasi yake, muda wa watoto kutambulika na kujulikana, ubaki pale pale,” alisema mama Alikiba.

Mamake Alikiba afunguka makubwa kuhusu maisha ya utoto ya mwanawe.

Kwa mara ya kwanza, mama yake na msanii Alikiba amefunguka jinsi msanii huyo alijipata katika tasnia ya muziki ambako amedumu kwa Zaidi ya miaka 10 sasa.

Mama Alikiba ambaye si rahisi kuonekana kwenye vyombo vya habari safari hii alizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake na kufichua kwamba Alikiba alianza kuupenda muziki akiwa na umri wa siku saba tu duniani.

Mma huyo wa wasanii Alikiba na Abdukiba alisema kuwa yeye hujitenga sana mbali na mitikasi ya wanawe na ndio njia moja ya kujizolea heshima.

“Kila kitu kipewe nafasi yake, muda wa watoto kutambulika na kujulikana, ubaki pale pale,” alisema mama Alikiba.

Vile vile alitumia fursa hiyo kuwashukuru wote ambao wanamppa sapoti mwanawe katika tasnia ya muziki kwa moja moja au nyingine ikiwemo kumtangaza.

“Kwanza nimpe Mungu shukrani kwa kuwapa wanangu kipaji ambacho leo kimetubadilishia maisha. Na ni muda mrefu amekuwa kwenye tasnia ya muziki, niwashukuru wote ambao wamemshika mkono kwa kumtangaza. Alikiba babake alikuwa dereva alimletea kaseti kipindo hicho akiwa na siku saba. Alipompa ile kaseti, Ali alichezesha kichwa. Tukaweka mshangao kwamba duh, mtoto anacheza mziki...” mamake Alikiba alisema.

Baadae katika ukuaji wake, Alikiba akiwa na miaka 3 alikuwa anaambatana na mama mmoja kwenda katika shughuli za harusi na ulipokuwa unafika muda wa muziki, mtoto Ali alikuwa anawaacha wengi vinywa wazi kwa kucheza muziki bila haya.

Mahojiano hayo na mamake Alikiba ni moja kati ya maandalizi kuelekea shoo kubwa kabisa ya Rocking 255 kule Masaki ambapo Alikiba atatumbuiza na msanii kutoka Nigeria Ayra Starr mnamo Mei 20 mwaka huu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved