logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkewe DK Kwenye Beat afunguka alivyohisi baada ya mumewe kutuhumiwa kwa ubakaji na kuwa na STD

DK  alimhakikishia kuwa kila kilichokuwa kikienezwa ni uongo.

image
na Radio Jambo

Burudani28 April 2023 - 12:08

Muhtasari


  • Wakizungumza na Diana Marua na mumewe Bahati, wanandoa hao walisimulia jinsi shutuma hizo zilivyoathiri taswira yao na kazi ya DK.

Msanii wa nyimbo za injili David Kilonzo almaarufu DK Kwenye Beat na mkewe Shanice Wangechi hatimaye wamezungumzia kashfa iliyotokea miaka minne iliyopita.

Kashfa hiyo ilihusu madai kuwa DK Kwenye Beat na Hopekid ambaye pia ni mwanamuziki wa Injili walilala na mwanadada mmoja na mmoja wao kumwambukiza ugonjwa wa malengelenge.

Wakizungumza na Diana Marua na mumewe Bahati, wanandoa hao walisimulia jinsi shutuma hizo zilivyoathiri taswira yao na kazi ya DK.

Shanice alikuwa akifanya kazi nchini Qatar wakati huo lakini habari zilienea sana hivi kwamba wenzake ambao pia walikuwa Wakenya walianza kuizungumzia.

Alifichua kuwa habari hizo zilimshtua sana lakini alichagua kumsikiliza DK na kuamini chochote alichomwambia.

DK  alimhakikishia kuwa kila kilichokuwa kikienezwa ni uongo.

Hakuwa na la kufanya zaidi ya kumwamini mume wake kwa sababu hakuwahi kumpa sababu yoyote ya kumtilia shaka kwa miaka yote waliyoishi pamoja katika mahusiano na ndoa.

Ikabidi DK aende kufanyiwa vipimo ili kuthibitisha kuwa hakuwa na ugonjwa wa STD kwa sababu wazazi wa Shanice walikuwa na wasiwasi juu yake hasa kwa kuwa ni mtoto wao wa pekee na virusi vinaua.

Wawili hao walisaidiana katika kipindi chote cha kushambuliwa mtandaoni na baadaye wakabarikiwa  na binti mrembo ambaye sasa ana umri wa miaka miwili.

“Mwaka 2018 mambo yalikuwa mazuri, halafu Januari 2019, ikawa nzuri pia kwa sababu hiyo ilikuwa ni awamu mpya kaka yangu alikuwa anaingia shule na mimi ndiye mlezi.

Mungu amekuwa mwaminifu na niliweza kumpeleka shule ya bweni. Nilisisimka sana. Halafu ikafika Februari."

Wakati huo ilikuwa ni shutuma kutoka kwa blogu, kwamba msanii ametoa herpes pamoja na kumbaka mwanamke.

"Nitaishi kukumbuka lakini hiyo ndiyo siku niliyokutwa na kashfa, kashfa ya majaribio. Huo ukawa mwanzo wa msitu mpya kwangu"

Tangu wakati huo hadi sasa, mambo hayajawahi kuwa sawa tena. Aliongeza

"Scandal ilinipata mnamo 2019 Feb, na hii ni kashfa ambayo si kitu cha kawaida, sijawahi kuwa na kashfa ya huduma na kazi, na niko kileleni, mambo yalikuwa mazuri"

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved