logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Fatxo avunja kimya mitandaoni, "Nimesimama tena!"

Mwanamziki DJ Faxto amejitokeza kwa umma baada ya uchunguzi wa kifo cha Jeff Mwathi kukamilika.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 May 2023 - 11:58

Muhtasari


  • • Mwathi, 23, alikufa mnamo Februari 22, 2023 baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya 10 ya jengo analoishi DJ Fatxo.
  • • Mwanamziki maarufu wa muziki ya Muguthi DJ Faxto amejitokeza kwa umma kwa mara ya kwanza baada ya uchunguzi wa kifo cha Jeff Mwathi kukamilika.
DJ Faxto anayeshukiwa kwa kifo cha Mwathi

Mwanamziki maarufu wa muziki ya Muguthi DJ Faxto amejitokeza kwa umma kwa mara ya kwanza baada ya uchunguzi wa kifo cha Jeff Mwathi kukamilika.

Mwathi, 23, alikufa mnamo Februari 22, 2023 baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya 10 ya jengo analoishi DJ Fatxo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Fatxo alitangaza kurejea kwake akisema yeye ni kama ndege iitwayo Phoenix, ambayo hupepea licha ya changamoto zinazotupwa njiani pake.

"Na kama vile Phoenix alipoinuka kutoka kwenye majivu, nitasimama pia!” Faxto alisema.

Faxto ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi majuzi aliwasihi wakenya kumuombea akisema kuwa mwaka wa 2023 umekua mgumu kwake.

“Kurudi kutoka kwa miale ya moto, bila kuvikwa chochote ila nguvu na ushindi wa ajabu kuliko hapo awali.” Faxto aliongeza.

“Wahandisi wa Kanisa la KAG mumebarikiwa, asante kwa mapokezi mazuri." Alitangaza

Maafisa wa upelelezi ambao wamekuwa wakichunguza kifo hicho tatanishi cha Mwathi nyumbani kwa mwimbaji wa Benga DJ Fatxo wanasema hakukuwa na ushahidi wa kimahakama unaoonyesha kwamba marehemu mbunifu wa mapambo aliuawa.

Kulingana na matokeo ya wapelelezi, kutokuwepo kwa Mwathi kuligundulika saa chache baada ya kushindwa kuamka, jambo lililosababisha ukaguzi katika chumba alichokuwa amelala.

Wapelelezi wanaamini Mwathi aliruka kutoka dirishani, jambo ambalo linaweza kueleza ni kwa nini mwili wake uligunduliwa na suruali yake kwenye goti, mara yake ya mwisho kugusa dirisha ilikuwa kiunoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved