logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nilikuwa maarufu kumliko na sivutiwi na pesa zake" - Ex wa Hakimi awajibu wakosoaji

Alisema talaka ilichochewa na uvumi wa Hakimi kumbaka mwanamke kwenye kitanda chao.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 May 2023 - 11:06

Muhtasari


  • • Abouk alisema kwamba kutaka talaka hakukuwa na kusudi lolote la kutaka mgao katika mali ya mchezaji huo.
  • • Talaka yake ilichochewa na uvumi kwamba Hakimi alimbaka mwanamke kwenye kitanda cha ndoa wakati mkewe na watoto wamenda ziara Dubai.
Mke wa Hakimi amevunja ukimya kufuatia sakata la talaka na kukosa mali.

Hiba Abouk, mke wa zamani wa mwanasoka wa Morocco Achraf Hakimi, amekuwa akichukua vichwa vya habari hivi karibuni.

Mwigizaji na mwanamitindo huyo sasa ameibua mapya baada ya kudai kuwa alikuwa maarufu zaidi kuliko mwanasoka huyo walipoanza kuchumbiana mwaka wa 2018.

Hata hivyo, madai haya yamezua utata mwingi, hasa kwa vile alidaiwa kutaka nusu ya utajiri wake baada ya talaka yao.

Abouk amesema kuwa hana nia ya utajiri wa mchezaji huyo, lakini inaonekana watu wengi hawajashawishika na hilo.

Kulingana na ripoti, mwigizaji huyo anadaiwa aligundua kuwa Hakimi alikuwa amesajili mali yake yote kwa jina la mamake. Hii imechochea mjadala kuhusu kama Abouk ana haki ya kupata mgao wa nyota huyo wa PSG.

Licha ya upinzani huo, Abouk anasalia imara katika msimamo wake. Katika mahojiano na mwanahabari Maria Patino kupitia AS, mwigizaji huyo alinyoosha maelezo baada ya kutupiwa swali hilo akisema;

"Habari, María. Ni ulimwengu uliojaa chuki za wanawake tunamoishi. Kwa kuzingatia kwamba, tulipoanzisha uhusiano, hakupata pesa na mimi nilijulikana zaidi kuliko yeye.”

Maoni ya Abouk yamezua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii, huku watu wengi wakitoa maoni yao kuhusu suala hilo. Baadhi wamemkosoa kwa kudai sehemu ya mali ya Hakimi, huku wengine wakiunga mkono madai yake kwamba alikuwa maarufu kuliko yeye walipoanza kuchumbiana.

Baada ya kutoa tamko hilo, aliyekuwa mumewe Hakimi Jumapili alipakia picha ya pamoja wakiwa na mamake na kumwandikia ujumbe wa kumsherehekea siku ya kina mama, akimtaja kama mhimili muhimu katika maisha yake.

Inabakia kuonekana jinsi hali hii itakavyokuwa, lakini jambo moja ni la uhakika: utata unaozunguka talaka ya Hakimi na Abouk hautaisha hivi karibuni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved