logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya seneta Karen Nyamu kuonekana akitafuna miraa

Mama huyo wa watoto watatu alishangaa kwa nini hadithi za miraa huwa za kuvutia.

image
na Samuel Maina

Burudani10 May 2023 - 06:41

Muhtasari


  • •Seneta huyo wa UDA alionekana pamoja na wanaume kadhaa ambao alionekana kuwa na wakati mzuri nao.
  • •Makumi ya wanamitandao walikuwa wepesi kushiriki maoni yao kuhusu mada iliyoibuliwa na seneta huyo.

Siku ya Jumanne, seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu alichapisha picha yake ya kumbukumbu akitafuna miraa.

Pichani, alionekana pamoja na wanaume kadhaa ambao alionekana kuwa na wakati mzuri nao. Alionekana akiwa ameshika mfuko unaoaminika kuwa na mihadarati hiyo huku tayari akiwa na tawi moja mdomoni.

Katika maelezo ya picha hiyo, mama huyo wa watoto watatu alishangaa kwa nini hadithi za miraa huwa za kuvutia.

"Lakini mbona story za jaba (miraa) huleta shangwe hivyo," alihoji.

Kama kawaida, makumi ya wanamitandao walikuwa wepesi kushiriki maoni yao kuhusu mada iliyoibuliwa na seneta huyo.

Tazama baadhi ya maoni ya Wanamitandao:-

Triza Wainaina: Huwa sielewi juzi nilikaa next kwa gari chali wawili wakichana story nazo mpaka nikafeel vibaya wakishuka but sielewi kitu sheg Nayo 🤣 .

Janet Jayna: Hapa najua mlikuwa mshanunua KICC na mkaiuza aki zikishika zimeshika.

Swit Angel K-lyn: Napenda jinsi unavyoishi maisha yako ya kweli bila kujifanya.

Hottensia Kaka: Kila kijiti na story yake.

Load App: Hio sasa ndio hufanya Samidoh asikuache. Vibe ingine haieleweki mathigithanio kadame roho safi, vituko hakana tumaringo uko tuu kitu haii sijui.

Senetor Karen Nyamu sio mgeni kwa utata. Anajulikana sana hasa kutokana na drama nyingi ambazo zimezingira maisha yake.

Katika miaka ya hivi majuzi, umakini mkubwa umekuwa kwenye mahusiano yake yenye drama nyingi na mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh. Wawili hao wanaaminika kuwa wapenzi na hata wana watoto wawili pamoja.

Katika miaka ya hivi majuzi, umakini mkubwa umekuwa kwenye uhusiano wake wenye utata na mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Mke wa mwimbaji huyo wa nyimbo za Kikuyu, Edday Nderitu hata hivyo amekuwa akipinga suala la mume wake kuwa na wake wengi.

Takriban miezi mitatu iliyopita, Edday alimwandikia Samidoh ujumbe mrefu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimuonya kwamba hayuko tayari kamwe kulea watoto wao katika ndoa ya wake wengi.

Hii ilikuwa baada ya mwanamuziki huyo kuonekana na Nyamu licha ya seneta huyo awali kudai uhusiano wao umefika mwisho.

Edday alimtaja Bi Nyamu kama mtu asiye na maadili na asiyeheshimu familia yake. Alidokeza kuwa takriban miaka mitatu iliyopita ya ndoa yake imejawa na maumivu na fedheha nyingi. Hata hivyo, alisema licha ya yote amebaki mwaminifu na ameendelea kuunga mkono kazi ya msanii huyo wa nyimbo za Kikuyu. 

"Umenifanya nionekane mjinga na kuchukulia ukimya wangu kuwa wa kawaida, nimekusaidia kuinua kipaji chako na kukuunga mkono kwa yote, lakini kitu kimoja nimekwambia na nasema hapa tena sitalea watoto wangu katika familia ya wake wengi," Edday alimwambia mwanamuziki huyo mwezi Februari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved