Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 30 ameelekea mahakamani akimshataki rapa mkongwe na mjasiriamali wa Marekani, Jay-Z akidai kuwa ni babake aliyemtoroka.
Rymir Satterthwaite, 30, amesisitiza kuwa hataki chochote kutoka kwa rapa wa Empire State of Mind, ambaye kwa sasa ameoana na Beyonce, zaidi ya kutambuliwa tu!
Kulingana na DailyMail.com, alidai kuwa marehemu mamake, Wanda, alikuwa kwenye uhusiano wa kizamani na mwanamume mwingine alipofanya mapenzi na bilionea huyo mwaka 1992, alipokuwa na umri wa miaka 16 na yeye akiwa na miaka 22.
Kufikia wakati alipozaliwa Julai iliyofuata, mapenzi yao ya muda mfupi yalikuwa yameisha, na alikuwa ameorodhesha mchumba wake wa utotoni - Robert Graves - kama baba yake kwenye cheti chake cha kuzaliwa.
Alidai kuwa mama yake alimwambia kuwa Shawn Carter – jina halisi la Jay-Z, mwenye umri wa miaka 53, ndiye baba yake halisi akiwa na umri wa miaka minane, na ametumia miaka mingi kuthibitisha hilo.
Mapema mwaka huu, ombi lake la kutaka hati za mahakama zifunguliwe lilikataliwa na Mahakama ya Juu ya New Jersey.
Chombo hicho kinaripoti kwamba sasa amehamia kuwasilisha tena hii kwa Kitengo cha Rufaa cha Mahakama ya Juu ya New Jersey, na kwa sasa inazingatiwa.
Inasemekana kwamba Wanda – mamake, aliomba kwamba Jay na Robert wafanye mtihani wa uzazi huko Pennsylvania mwaka wa 2010, ambapo ilithibitishwa kuwa baba huyo (Robert) hakuwa na uhusiano wa kibaolojia na mtoto wake wa kiume na jina lake liliondolewa kwenye cheti cha kuzaliwa - ambacho sasa kinasemekana kuwa hakijaandikwa jina la 'baba'.
Rymir alidai kuwa timu ya nyota huyo ilijaribu kupotosha mfumo wa kisheria ili kuepuka vpimo vya kujua baba halali, na kupeleka juhudi zake kwenye Mahakama ya Juu - na hati hizo zimeripotiwa kuonekana na majarida.