'Nahitaji msaada!,'Mc Fullstop azungumza baada ya kudaiwa kufariki

Alidokeza kwamba hajisikii sawa na kuwashukuru wale ambao wamekuwa wakisimama naye wakati wa ugonjwa wake.

Muhtasari
  • Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa imeripotiwa kuwa mshukiwa huyo alitumia nembo ya Citizen TV Kenya kudai kuwa Mc huyo mashuhuri amefariki dunia.
  • Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mc fullstop, alidai kuwa anakwenda kumchukulia hatua mtuhumiwa huyo.
Mc Fullstop
Image: HISANI

Mtangazaji mashuhuri wa Reggea, John Maina almaarufu MC Fullstop ameomba usaidizi wa kumtafuta mshukiwa ambaye amekuwa akidai kuwa amefariki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa imeripotiwa kuwa mshukiwa huyo alitumia nembo ya Citizen TV Kenya kudai kuwa Mc huyo mashuhuri amefariki dunia.

Akitumia akaunti zake tofauti za mitandao ya kijamii kutoa maoni yake kuhusu mada hii, MC FULLSTOP amemtaja mwanamume huyo ambaye alisema amekuwa akifanya hivyo kwa muda.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mc fullstop, alidai kuwa anakwenda kumchukulia hatua mtuhumiwa huyo.

"Amenizuia tu! Ila bado tunaweza kumpata, sio first time nimefanya hivi but saa hii ame affect my whole family, wameshtuka, panic wazee ndio mmeathirika sana. @DCI_Kenya@NPSOfficial_KE@PolisiKE NAHITAJI MSAADA!" Aliongea Fullstop.

Wakati wakijibu kisa hicho, Wakenya waliotumia akaunti zao tofauti za mitandao ya kijamii kutoa maoni yao kuhusu madai haya wameitaka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai kumsaidia DJ huyo kumpata mshukiwa.\

Mwezi mmoja uliopita Mtangazaji huyo maarufu wa nyimbo za Reggea na Dancehall alibainisha kwamba anapata shida sana kukimbia, kutembea na hata kuzungumza baada ya ugonjwa huo kuathiri mapafu na koo lake.

"Hii imeenda” kwa kweli. Pafu langu la kushoto limeanguka kabisa nimebaki na moja," alisema kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Aliongeza, "Mwaka wa 2021 niligunduliwa na TB ya mapafu ikakula mapafu kabisa. 2022 nikapata TB ya koo nayo ikanimaliza sauti. Kukimbia, kutembea na kuongea ni shida,"

Maina aliambatanisha ujumbe huo na picha yake akiwa amelala kwa kitanda cha hospitali huku akiwa anawekwa hewa kupitia mrija ambao uliwekwa kwenye pua lake na picha nyingine ya X-ray iliyoonyesha jinsi pafu lake limeathirika.

Alidokeza kwamba hajisikii sawa na kuwashukuru wale ambao wamekuwa wakisimama naye wakati wa ugonjwa wake.

"Alafu mapafu yana ufala sio kama ini, haiwezi kujiponya itabidi nijipange hapa naona niki hang boots. Nataka tu kusema asante kwa wale wamekuwa wakinisapoti katika kipindi hiki kigumu Mungu awabariki sana," alisema.