Taarifa ambazo hazijadhibitishwa kikamilifu zinadai kwamba Charlotte Powdrell, mpenzi waliyeachana na mwanabondia Israel Adesanya raia wa New Zealand mweney usuli wa Nigeria, ameripotiwa kumburuza mahakamani na kutaka nusu ya mali yake akabidhiwe yeye licha ya kutokuwa kweney ndoa naye.
Mpiganaji wa UFC Sean O'Malley alifichua hili alipokuwa akizungumza kwenye podikasti iliyotiririshwa kwenye chaneli ya Suga ya YouTube.
Alisema msichana husika hakuwahi kuolewa na Israel wala hakuwa na mtoto naye lakini anaamini ana haki ya nusu ya utajiri wake kwa sababu "walichumbiana kwa muda mrefu sana na aliunga mkono taaluma yake ya Ultimate Fighting Championship, UFC."
O’Malley alisema, “Mpenzi wa zamani wa Izzy [Israel Adesanya]…Hawajaoana, sawa hawakuwahi kuoana sikuamini. Anataka nusu ya mali yake. Sijui uhusiano wao ulikuwaje kwa sababu sikujua hata alikuwa na rafiki wa kike, lakini kutaka nusu ya kile alichotoka na kufanya ni ujinga kabisa."
Uhusiano wa Adesanya na Charlotte Powdrell ulikuja kujulikana mnamo 2019 baada ya kuonekana pamoja baada ya ushindi wake dhidi ya Robert Whittaker.
Powdrell ni wakala wa mali isiyohamishika wa New-Zealander aliyeko Auckland.
Israel Adesanya ndiye bingwa wa sasa wa UFC uzito wa Middleweight na mmoja wa wasanii wa karate wanaolipwa zaidi duniani.
Sakta hili la mpenziwe kutaka nusu ya mali yake linakuja mwezi mmoja baada ya mpenzi wa mwanasoka wa Morocco, Achraf Hakimi, Hiba Abouk kudaiwa kuelekea mahakamani pia akidai nusu ya mali ya kijana huyo ambaye Hiba amemshinda kwa miaka 12.
Kwa kustaajabu, inadaiwa Hiba alipata Hakimi amemuandikishia mali yote mamake na yeye hakuwa na mali yoyote katika jina lake.