logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Alikiri hajui chochote!" Mwalimu wa kiingereza Diamond Platnumz avunja kimya

Diamond pia alimuomba Allan kuwafundisha wasanii wake wengine katika WCB.

image
na Samuel Maina

Burudani16 May 2023 - 05:19

Muhtasari


  • • Tr Allan amemtaja mwimbaji huyo kuwa ni mwanafunzi mwenye bidii na ambaye yuko tayari kujifunza.
  • •Diamond pia alimuomba Allan kuwafundisha wasanii wake wengine katika WCB.

Mwalimu wa Kiingereza wa Diamond Platnumz, Tr Allan amemtaja mwimbaji huyo kuwa ni mwanafunzi mwenye bidii na ambaye yuko tayari kujifunza.

 “Mimi ni mwalimu wa Kiingereza wa Diamond Platnumz,” aliiambia Bongo 5.

Allan alisema kuwa mwimbaji huyo alimfikia alipoanza kwenda kimataifa.

"Aliniambia alitaka kufundishwa Kiingereza na hasa Kiingereza cha Marekani. Alikiri kwamba hajui chochote."

 "Nilianza kumfundisha mambo ya msingi, sasa hivi anazungumza Kiingereza kizuri sana hadharani."

Diamond pia alimuomba Allan kuwafundisha wasanii wake wengine katika WCB.

"Nilimfundisha Rayvanny, Harmonize na wengine wengi," alisema Allan.

Diamond alitambulishwa kwa mwalimu Allan na aliyekuwa mpenzi wake Penny.

"Alikutana na mimi kupitia mpenzi wake wa zamani Penny. Alipoachana na Wema Sepetu, alianza kutoka na Penny na hivyo akatuunganisha," Allan alisema

Aliongeza; "Alinilipa vizuri, ni mtu mkarimu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved