Mwanamziki wa nchi ya Tanzania Marioo amewaomba mashabiki wake kumuombea baada ya kuugua.
Mwanamziki huyo ambaye aliwatumbuiza mashabiki wake Jumamosi tarehe 13, Mei amelazwa hospitalini.
Alichapisha katika mtandao wake wa Instagram akisema kuwa aliwashukuru mashabiki wake kujitokeza katika shoo yake.
“Nawashukuru wote Mliojitokeza kuja kunisupport kijana wenu. Ama hakika shughuli ilifana sana 🙏🏽 japo Niliumwa sana kuanzia usiku wa juzi mpaka usiku wa Tukio Yaani Mpaka saa 6 usiku Bado nimelazwa hospitalini,” aliandika Mario
Licha ya kuumwa usiku mzima msanii huyo bado ailiwatumbuiza mashabiki.
Msanii huyo alichapisha video katika akaunti yake ya Instagram akiwa amelazwa hospitalini.
Mwanamziki huyo pia alimshukuru mpenzi wake wa hivi majuzi Paula Kajala na mama mkwe wake Fridah Kajala kwa kuwa naye mpaka kupata nafuu.