logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari amhakikishia mumewe kuhusu upendo wake kwake baada ya kushambuliana na Diamond

Zari alishtumu aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz kwa kuharibu ndoa yake changa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 May 2023 - 13:40

Muhtasari


  • •"Kwa mume wangu ... nilikuchagua wewe kwa wanaume wote. Imiliki na ujivunie ... usiruhusu wasiwasi wa mapenzi uharibu tulichonacho ... kwa upendo Bi Lutaaya," aliandika mke wake Shakib.
Zari aandikia mumewe ujumbe wa kuthihirisha mapenzi yake kwake

Baada ya drama zote zilizotokana na filamu ya Young, Famous and African, mwanasosholaiti wa Uganda, Zari Hassan aliandika ujumbe wa kuthibitisha upendo wake kwa mumewe mdogo, Shakib Cham Lutaaya kwenye Instastory yake.

"Kwa mume wangu ... nilikuchagua wewe kwa wanaume wote. Imiliki na ujivunie ... usiruhusu wasiwasi wa mapenzi uharibu tulichonacho ... kwa upendo Bi Lutaaya," aliandika mke wake Shakib.

Hii ni baada ya aliyekuwa mpenzi wake na mzazi mwenzake Diamond Platnumz kuibua madai kwamba bado Zari  anampenda na hata alitaka kupata mtoto mwingine naye.

Siku chache zilizopita mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42, alishtumu aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz kwa kuharibu ndoa yake.

Baadaye Zari alidokeza kuwa madai ya staa huyo wa Bongo dhidi yake yalisababisha mgogoro katika ndoa yake mpya na Shakib.

Katika tukio moja kwenye filamu ya uhalisia iliyoachiwa siku ya Ijumaa, Young, Famous and African sehemu ya pili, Diamond Platnumz alisikika akimwambia mshikaji wake mpya, Francine Koffie almaarufu Fantana kutoka Ghana kwamba mpenzi wake wa zamani Zari Hassan alitaka mtoto wa tatu naye.

Katika majibu yake yaliyojaa machungu, Zari Hassan alikanusha madai kuwa bado anampenda mwimbaji huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 32 na kwamba aliomba kuzaa naye mtoto mwingine.

Mwanasosholaiti huyo alidai kuwa Diamond ndiye amepata ugumu wa kusonga mbele baada ya. mahusiano yao kuvunjika.

Kutokana na hayo, aliweka wazi kuwa uhusiano wao hautakuwa sawa tena na kubainisha kuwa anaweza kujisimamia mwenyewe.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved