logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Peter Drury amtakia heri Arap Uria akiendesha baiskeli kutoka Eldoret hadi Nairobi

"Safari imezidi kuwa ngumu lakini nitaikamilisha kesho. Mwisho ni kwenye Barabara ya Bunge," Arap alisema Jumatatu.

image
na Radio Jambo

Habari30 May 2023 - 05:19

Muhtasari


•Arap anatumai kukamilisha safari hiyo ngumu ambayo imemchukua siku kadhaa hivi leo, Jumanne anapotarajia kuwasili Nairobi.

•Arap alieleza ombi lake kwamba waziri wa michezo Ababu Namwamba awe katika Barabara ya Bunge kumkaribisha anapowasili.

amejawa bashasha baada ya Drury kumtakia heri akiendesha baiskeli kutoka Eldoret hadi Nairobi

Wiki iliyopita, mchekeshaji Arap Uria alianza safari kutoka Eldoret hadi Nairobi kwa baiskeli katika hatua ya kutimiza ahadi aliyokuwa ametoa.

Shabiki huyo wa klabu ya soka ya Chelsea diehard iiapa kuendesha baiskeli kwa safari hiyo ya zaidi ya kilomita 300 iwapo timu hiyo aiipendayo ingeshindwa na Manchester United katika mchuano wao mkubwa wa Mei 25.  Ndani ya dakika 90 za mechi hiyo, The Blues walipokea kichapo cha  4-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Arap anatumai kukamilisha safari hiyo ngumu ambayo imemchukua siku kadhaa hivi leo, Jumanne anapotarajia kuwasili Nairobi.

"Safari imezidi kuwa ngumu lakini nitaikamilisha kesho. Mwisho ni kwenye Barabara ya Bunge," alisema siku ya Jumatatu.

Kulingana na taarifa zake za moja kwa moja, mchekeshaji huyo alivuka hadi kaunti ya Kiambu Jumatatu na akasimama Limuru.

Pia alionyesha ujumbe mzuri kutoka kwa mtangazaji maarufu wa soka Peter Drury ambaye alimtakia heri katika safari yake.

"Habari Arap, ni Peter hapa, nakutakia kila la kheri kwenye safari yako kubwa ya kuelekea Nairobi. Uwe salama, furahia na ninatazamia kuzungumza nawe tena," Drury alisema kwenye video ambayo Arap alishiriki kwenye Facebook.

Arap aliyeonekana kufurahishwa sana na ujumbe wa Drury aliusherehekea na kumshukuru kwa maneno yake mazuri.

"Tunahitaji marafiki kama hawa maishani. Asante sana Peter Drury. Mwisho ni kesho katika Barabara ya Bunge saa sita adhuhuri," Arap alisema Jumatatu.

Mchekeshaji huyo pia alieleza ombi lake kwamba waziri wa michezo Ababu Namwamba awe katika Barabara ya Bunge kumkaribisha anapowasili jijini Nairobi Jumanne. Tunamtakia Arap kila la heri anapoendelea na safari yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved