Video ya wanandoa mashuhuri, Kelvin Bahati na Diana Marua wakibadilishana mavazi na majukumu imezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii.
Jumatano, Diana Marua alichapisha video iliyomuonyesha kiwa amevalia nguo za mwanaume huku Bahati akiwa amevalia gauni. Katika video hiyo, alionekana akimsumbua mumewe ambaye alikuwa akiigiza nafasi ya mwanamke nyumbani.
Bahati ambaye kwenye video alionekana kukerwa na usumbufu wa mkewe alisikika tu akilalamika na kumuomba aache.
"Mume wangu Bahati sasa anaelewa inavyohisi kuwa mwanamke kwenye mahusiano .. awww Staaap it," Diana alisema.
Miongoni mwa mambo yaliyoonekana kwenye video ni pamoja na Bahati akisafisha vyombo jikoni, akifanya usafi, akifanya kazi na kompyuta huku Diana Marua akipumzika na kucheza mchezo wa video.
Video hiyo imevutia kila aina ya maoni, mengine ya kufurahisha, mengine mazuri na hata maoni mengine mabaya.
Tazama baadhi ya maoni:
kezziecire Kama si hivi sitaki. Muoe marafiki wenu bora. Hiyo ndiyo siri.
okello_sejo Mtu aite kikosi cha uokoaji. Mwanaume mmoja yuko chini.
@boss_emanu Hii ni kunyanyaswa. Maskini BahatI
@skppre Mwanaume chini
@wANJI001 Ukioa mwanamke mzee kukuliko.
@Kenny_Kyp Hili ndilo jambo la kuchukiza zaidi kuwahi kutazama. Nafikiria, ikiwa wanaume wote watafanywa kuwa wanawake, basi kizazi cha baadaye cha mwana kitakuwaje? Je, wanaweza kutengeneza uzio, kujua misumari sahihi ya kuweka mabati, inchi, kuweka mshale wa mnyororo, kulisha ng'ombe nk? Au watakuwa kwenye manicure ya wigi?
@kuwamocho_ Kuwa mashuhuri hapa Kenya ni ngumu, unalazimika kujipunguza hadi hapa ndio ubaki wa maana.
Tazama video:-
Maoni yako ni yepi?
Wakizungumza katika video iliyochapishwa kwenye mtandao wa YouTube mwezi Aprili, Diana Marua alifichua kwamba hakuwa tayari kwa ndoa wakati alipokutana na mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili.
Mama huyo wa watoto watatu alidai kwamba Bahati alimnasa kwenye ndoa yao ya sasa kwa kumtunga ujauzito katika mwezi wa saba wa uchumba wao.
Ulininasa katika mwezi wa saba. Ulininasa. Lakini mpenzi ulikuwa unanipenda. Ulikuwa unakuja na hiyo Mercedes ya bluu kutoka Ruaka hadi Syokimau. Sijui mbona ulikuwa unakuja kwangu saa sita usiku," Diana alisimulia.
Kwenye mazungumzo hayo, Bahati alibainisha alimsaidia mwanavlogu huyo kuacha maisha ya anasa na kuanzisha familia.
"Kama isingekuwa mimi, zile klabu zinafungwa zingekuwa zinafungwa ukiwa ndani. Ungekuwa huko tu unaserereka unauliza utapata watoto lini alafu unajibu 'bado niko mdogo'" Bahati alimwambia mkewe.
Aliongeza,"Mimi ndio nilikwambia haya mambo ya kuwa mdogo."
Diana Marua kwa upande wake alimweleza mwanamuziki huyo kwamba hangekuwa katika nafasi ambayo yuko kwa sasa ikiwa hangekuja katika maisha yake zaidi ya nusu muongo uliopita.
"Naweza kukuambia kitu? Unajua isingekuwa mimi, leo usingekuwa na nyumba hii. Isingekuwa mimi, usingepata watoto hawa. Isingekuwa mimi, usingekuwa na magari manne yameegeshwa hapa," Diana alimkumbusha Bahati.
Mama huyo wa watoto watatu alimweleza mwimbaji huyo kwamba usaidizi ambao amempa ni dhibitisho la kweli la mapenzi.