logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mulamwah amposti mzazi mwenzake Carol Sonnie kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu

Mulamwah na Sonnie walitangaza kutengana mwaka wa 2021 baada ya kuzaliwa kwa binti yao Keilah Oyando.

image
na Radio Jambo

Habari03 June 2023 - 10:54

Muhtasari


•Mulamwah alishiriki mabango mawili ya Sonnie kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa madhumuni ya kutangaza shoo ya TV.

•Hatua hiyo inaweza kuashiria kuwa pengine uhusiano wa wazazi wenza hao wa sasa ni mzuri licha ya kurushiana maneno makali hapo awali.

Mchekeshaji mashuhuri David Oyando almaarufu Mulamwah amechapisha picha ya mzazi mwenzake Carol Sonnie kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

Siku ya Jumamosi, baba huyo wa mtoto mmoja alishiriki mabango mawili ya Sonnie kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa madhumuni ya kutangaza shoo ya TV.

Sonnie ameratibiwa kuwa mgeni wa Diana Marua na Dr Ofeneke kwenye kipindi cha Mr Right Season 3 kwenye Rembo TV.

“Leo Usiku kwenye #HelloMrRight,” Mulamwah aliandika chini ya bango alizochapisha.

Ingawa chapisho hilo huenda lisiwe na maana kubwa, ni hatua ya kutatanisha ikizingatiwa uhusiano mbaya na drama zilizofuatia kusambaratika kwa mahusiano yao mwaka wa 2021. Pia inaweza kuashiria kuwa pengine uhusiano wa wazazi wenza hao wa sasa ni mzuri licha ya kurushiana maneno makali hapo awali.

Carol Sonnie amekuwa akiweka mahusiano yake siri huku Mulamwah akidaiwa kuchumbiana na rafiki yake Ruth K. Licha ya mara nyingi kuonekana wakijivijari pamoja kimahaba, wawili hao wamekuwa wakikanusha kuwa wapenzi.

Mapema mwaka huu, Mulamwah alibainisha kuwa uhusiano wake na 'bestie' wake Ruth K ni wa kirafiki tu.

Akizungumza na waandishi wa habari, mpenzi huyo wa zamani wa Carrol Sonnie aliweka wazi kuwa hakuna uhusiano wa kimapenzi kati yake na muigizaji huyo.

"Hakuna uhusiano ya kimapenzi kusema kweli. Namheshimu sana mpenzi wake. Ako na mpenzi," mchekeshaji huyo alisema.

Baba huyo wa binti mmoja alisema kwamba mpenzi wa Ruth ni rafiki yake mkubwa na hana tatizo lolote na urafiki wao.

Alifichua kwamba huwa anakutana mara kwa mara na mwanaume huyo na kushiriki mazungumzo ya kirafiki.

"Huwa tunakutana. Ni rafiki yangu. Hananga maneno, anaelewa hii biashara," alisema.

Katikati mwa mwaka jana, Sonnie alikuwa akijigamba kuhusu mahusiano mapya na kuonyesha  mpenzi wake mpya hadharani. Sonnie hata hivyo alikuwa akionyesha sehemu tu ya mpenziwe na kuficha sura yake.

"Niliamua na kusema wacha watu waone niko na furaha lakini wasione ni nani anafanya niwe na furaha. Hawahitaji kuona uso wake lakini niko na furaha sana," Sonnie alisema mwezi Agosti katika mahojiano na Nicholas Kioko.

Wakati huo, Muigizaji huyo alifichua kwamba  alikuwa amechumbiana na mpenziwe mpya kwa kipindi cha takriban miezi miwili.

Hata hivyo alidokeza kuwa yeye na  mpenzi huyo wake mpya wamekuwa marafiki kwa muda mrefu.

"Tumekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 10. Alikuwa nje ya nchi, alirudi miezi michache iliyopita," Alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved